VIWANGO VYA ELIMU YA LOWASSA NA MAGUFULI HIZI APA

By // No comments:

MH.EDWARD NGOYAI LOWASSA









GENERAL
SalutationHonourableMember picture
First Name: Edward
Middle Name:Ngoyai
Last Name:Lowassa
Member Type:Constituency Member
Constituent:Monduli
Political Party:CCM
Office Location:P.O. Box 139, Monduli
Office Phone: +255 754 800000
Ext.:
Office Fax: +255 22 2452037
Office E-mail: elowassa@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 26 August 1953
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
University of Bath, UKMSc. (Development Studies)--MASTERS DEGREE
University of Bath, UKMSc.19831984MASTERS DEGREE
University of Dar Es SalaamBA (Edu) Hons.19741977GRADUATE
Milambo Secondary SchoolA-Level Education19721973HIGH SCHOOL
Arusha Secondary SchoolO-Level Education19681971SECONDARY
Monduli Primary SchoolPrimary Education19611967PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
Tanzania GovernmentPrime Minister20052/8/2008
Ministry of Water and Livestock DevelopmentMinister20002005
State, Vice President's OfficeMinister for Environment & Poverty19972000
The Parliament of TanzaniaMember - Monduli Constituency19952015
Ministry of Lands, Human Settlement DevelopmentMinister19931995
State, Prime Minister's Office and First Vice PresidentMinister (Judiciary &Parliamentary Affairs)19901993
Arusha International Conference CentreManaging Director19891990
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember1990Todate
Chama Cha Mapinduzi, CCMParty Executive-District, Regional &Head Office19771989
























DR. JOHN POMBE MAGUFULI






Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.

Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.

Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.

Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.

Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)

Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.

Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).

Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali..











source;; JAMII FORUMS

KIPINDUPINDU,UAMBUKIZWAJI,DALILI,KUJIKINGA,NA MTIBABU

By // No comments:

Ugonjwa Wa Kipindupindu

   
Kipindupindu ni ugonjwa wa kuambukiza wa kuharisha unaosababishwa na vijidudu vya bakteria. Ugonjwa huu hutokana na matumizi ya maji yasiyo safi au chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi. Ugonjwa huu ni wa ghafla na kwa watu wengu hauleti dalili kali sana. Ingawa unatibika, kipindupindu kinaweza kuwa hatari sana na kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Maambukizi Ya Kipindupindu


Kipindupindu hutokana na maambukizi ya vijidudu vya bakteria viitwavyo Vibrio cholera. Vijidudu hivi hukaa kwenye majimaji, na wadudu kama nzi wanaweza kuvihamisha kutoka sehemu moja mpaka nyingine.
Maambukizi hutokea pale ambapo usafi wa maji, chakula, mazingira na binafsi haujazingatiwa. Kwa njia ya chakula vijidudu huingia kwenye utumbo na kisha kushambulia seli za utumbo. Dalili huanza kujionesha masaa 24 mpaka 48 baada ya maambukizi kutokea.

Dalili Za KIpindupindu


Kipindupindu huanza dalili masaa 24 mpaka 48 baada ya maambukizi. Huanza ghafla kwa kuharisha sana bila maumivu yoyote ya tumbo. Mwanzoni choo kinaweza kuwa kizito kidogo lakini baade kuwa chepesi kama maji, muonekano wako hufanana na maji ya mchele (maji baada ya kuosha mchele). Mgonjwa anaweza kuharisha mara nyingi sana kiasi cha kupata choo kwa mfululizo.
Baadae anaweza akaanza kutapika, akapata maumivu ya tumbo,kulegea na mwili kukosa nguvu kutokana na kupoteza maji na madini mengi sana.
Mara nyingi kipindupindu hakiambatani na homa. Wagonjwa wengi hupata dalili ambazo sio kali sana na kupona baada ya matibabu, wengine hupata dalili kali ambazo huchangia upungufu wa maji na mgonjwa kufariki.

Matibabu Ya Kipindupindu


Endapo unahisi una kipindupindu au kuna mtu ana kipindupindu basi wahi au mwahishe hospitali haraka!. Matibabu ya haraka ni muhimu kwa mtu mwenye ugonjwa wa kipindupindu. Kwa kiasi kikubwa ugonjwa hutambulika kwa dalili zake na uchunguzi wa daktari kwa mgonjwa. Pale unapojulikana matibabu ni muhimu ili kuzuia madhara yake. Kwa sababu ugonjwa huu huambukizwa kirahisi kwa njia ya maji na chakula, wagonjwa hutibiwa kwa kuwekwa sehemu za peke yao ili wasiambukize wengine.
Kumuongezea maji ni sehemu  muhimu ya matibabu kutokana na kupoteza maji mengi kwa kuharisha. Maji hupewa kwa njia ya mdomo kama ORS na kwa maji ya dripu.
Dawa kama Tetracycline, Ciprofloxacin na Doxycycline hutumika kwenye kutibu kipindupindu. Hizi zinasaidia kuua vijidudu vya kipindupindu ndani ya mwili.

Kujikinga na Kipindupindu


Usafi binafsi, chakula na mazingira ni muhimu ili kujikinga na kuzuia ugonjwa huu. Husambazwa kwa kutozingatia usafi na hivyo maji au chakula kuingiliwa na vijidudu vya ugonjwa huu. Ili kujikinga na kuzuia ugonjwa huu zingatia yafuatayo;
  • Nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni kila baada ya kwenda chooni
  • Nawa mikono kwa maji safi kabla na baada ya kula chakula au matunda.
  • Osha matunda kwa maji safi kabla ya kula
  • Tumia maji ya kunywa safi yaliyochemshwa au kutakaswa kwa dawa na kuhifadhiwa katika chombo kisafi.
  • Hakikisha unakula chakula ambacho hakijapoa. Kiwe cha moto na kimehifadhiwa katika chombo kisafi.
  • Tunza mazingira yako yawe katika hali ya usafi. Usiruhusu nzi kuruka ruka au kutua kwenye chakula chako.
DUMISHA USAFI WAKO WA NDANI NA MAZINGIRA YAKO PIA NA WEWE MWENYEWE BINAFSI..
POLE KWA TATIZO HILI LINALOKUSUMBUA NAAMIN UTAPONA KWANI KUUMWA SIO KUFA BALI KUTHIBITISHA KAMA KWELI WEWE UNA AFYA NZURI NA MWILI WAKO UMEWEZA KUTOA MAGONJWA YALIYOTAKA KUKUSHAMBULIA KATIKA MWILI WAKO...

FAHAMU NJIA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU YOYOTE YA VIUNGO VYA MWILI

By // No comments:

FANYA HIVI KUONDOA MAUMIVU YA MWILI WAKO NA UDUMISHE AFYA BORA KWA MWILI WAKO









Maumivu ya nyonga huweza kuandamana naya kiuno, nyonga huunganisha miguu na mifupa ya mapaja inayotengeneza kiuno. Nyonga ndiyo inayofanya utembee kutoka sehemu moja hadi nyingine,kukimbia,kuruka,kichurachura,n.k

Maumivu ya nyonga huwa makali na husambaa hadi kwenye magoti. Ukiwa na tatizo la nyonga huwezi kufanya shughuli nyingi, mfano kuchuchumaa. Kwa wanamichezo ni adui mkubwa wa ufanisi michezoni.

Mtu anaweza kupata maumivu ya kiuno iwapo ataanguka au   kupata ajali. Kiuno pia huweza kuumia kwa kuinama ghafla au kunyanyua kitu kizito. Watu wanaofanya kazi za kuinama ndiyo huathirika zaidi na tatizo hili.
Maumivu haya pia hutokea kwa kuumia vifupa vya nyonga ambapo vinaweza kuwa vimesagika au kuchoropoka. Matatizo ya nyonga pia hutokea kwa kuumia, kuteguka au kuvunjika. Uvujikaji unaweza kusababishwa na ajali yoyote, kwa kuanguka au kugongwa na gari, pikipiki au kitu kizito.
Magonjwa kama yabisi pia husababisha matatizo ya nyonga, saratani ya tezi dume kwa wanaume, saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake pia husababisha tatizo hili la kuvunjika nyonga endapo saratani hii itasambaa hadi ndani zaidi kwenye mifupa.

Kulingana na shirika la afya ulimwenguni (WHO), mtu mmoja katika ya wanane huvunjika nyonga kutokana na kuvuta sigara. Nae daktari wa mifupa anasema matumizi ya chumvi nyingi yanaweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa huo. Sababu za kuufanya mwili upoteze calcium kuwa ni kutumia kileo kupita kiasi ambacho huchangia kudhoofika kwa mifupa.

Kwa upande wa maumivu ya mgongo nyongani upande wa kushoto kuanzia juu ya makalio kwenda chini yanahusiana na mshipa wa fahamu uitwao sciatica.
Hii huwapata sana watu wanene wasiofanya mazoezi ya viungo. Isipotibiwa mapema huweza kusababisha mshituko wa moyo maana moyo unahusiana sana na mishipa ya fahamu kama vile ubongo, uti wa mgongo, ngozi na hisia pia.

MAZOEZI,
Watu wenye matatizo hayo wanapaswa kupatiwa mazoezi maalumu ili kuwasaidia kupona, kupunguza maumivu na kuwaepusha na matatizo kujirudia. Mazoezi yanayopendekezwa zaidi ni yale yanayofanywa bila kukaza sana mifupa na viungo.

Haya huanza kwa taratibu kwa mfano kutembea, kukimbia, kuogelea, kujinyoosha mara tatu au nne kwa wiki, kupanda ngazi, kucheza dansi na kuendesha baiskeli barabarani au zile maalumu zinazotumika kwenye nyumba za mazoezi (gym) Kwa upande wa kiuno na mgongo, mazoezi ni yale ya viungo maarufu kama “physiotherapy” kwa kutmia vifaa maalumu kama vile vya kujichua (massage).
Pia mazoezi mwengine ni ya kulala na tumbo kasha kuweka mikono mbele na kunyanyuka taratibu. Mgonjwa anapaswa kufanya hivyo mara kumi, pia mgonjwa aweke mikono upande akiwa amelala hivyo hivyo kasha anyanyuke taratibu afanye mazoezi haya mara kumi na mwisho aweke mikono nyuma mgongoni kasha anyanyuke tena mara kumi.

Mazoezi ya kupiga pushapu pia ni muhimu sana kwawatu wenye matatizo ya kuono na mgongo.

KUMBUKA;

  1. ·       Epuka kujitonesha kwa kufanya mazoezi haraka au kwa kutumia nguvu nyingi.
  2. ·       Epuka kubeba vitu vizito
  3. ·       Epuka kuinama ovyo au kazi ya kuchuchumaa
  4. ·       Jenga mazoezi ya kutembea mara kwa mara na epuka kukaa muda mrefu.
  5. ·       Iwapo kazi yako ni kukaa, jitahidi kila baada ya dakika 20 kunyanyuka na kutembea tembea
  6. ·       Punguza uzito
  7. ·       Kwa wanawake epuka kuvaa kiatu cha kisigino kirefu
  8. ·       Epuka kulalia godoro linalobonyea, tumia godoro maalumu la mgongo, ikiwezekana lala chini sehemu ambayo haibonyei.
  9. ·       Zingatia maelekezo ya daktari wako

FAHAMU WATU WENYE AKILI ZAIDI DUNIANI ( IQ )

By // No comments:

HAWA NDIO WATU WA KUWAANGALIA MAMBO YAO AMBAYO YATAKUNUFAISHA KATIKA ELIMU YAKO


 10.FABIANO LUIGI CARUANA.



9.MICHEAL KEVIN KEARNEY
Huyu ana historia ya kufanya kila kitu kabla ya muda.Ameanza kuongea akiwa na miezi minne,akajifunza kusoma akiwa na miezi kumi,Amemaliza high school akiwa na miaka sita na akapata degree yake ya kwanza akiwa na miaka kumi tu.



8.SAUL AARON KRIPKE.
Alijifunza kiyahudi akiwa na miaka sita na akajifunza kazi za wanafalsafa wengi sana wakubwa duniani.Akiwa bado yuko elimu ya juu ya sekandari aliitwa kufundisha chuo cha Havard kilichoko Marekani.Kwa sasa anachukuliwa kuwa mmoja kati ya wanafalsafa wakubwa duniani wa zama hizi.



7.AKRIT JASWAL.
Kijana huyu ana IQ ya 146 na wakati watoto wengine wanacheza michezo ya udaktari,yeye akiwa na umri wa miaka saba alishakuwa daktari na alifanya operation iliyofanikiwa vizuri kabisa.Kwa sasa anachukua degree ya hesabu.Kwasasa ni mtoto mwenye akili zaidi India na daktari wa upasuaji mdogo zaidi kuliko wote duniani.



6.RICK ROSNER.
Huyu ana IQ ya 192 na ni muandishi katika television ya MTV.Ameandika script nyingi ambazo ni mtu mwenye iq kama yake ndio anaweza kuandika la sivyo ingekuwa ngumu.



5.MISLAV PREDAVEC.
Huyu pia ana IQ ya 192.Pamoja na iq kubwa kiasi hicho ana maisha ya kawaida akiishi kama profesa wa hesabu na anabiashara ndogo tu.Ungeweza kudhani kuwa alipaswa kuwa tajiri namba moja duniani lakini amechagua maisha ya kuishi na familia yake na muda wote anapenda kukaa na mtoto wake wa kiume.





4.EIVANGEIOIS KATISIOILS.
Huyu ni mgiriki mwenye IQ ya 198 na ana phd.





3.MARILYN VOS SAVANT.
Huyu ana IQ ya kuanzia 160 mpaka 228(hakuna namba halisi inayofahamika) na ni muandishi,recture na muandishi wa makala za siasa za kufurahisha sana na za ukweli.





2.CHRISTOPHER MICHEAL LANGAN.
Mtu huyu ana IQ Ya 195 na alianza kuongea akiwa na miezi sita.Amekuwa na tabia ya kujifunza kila kitu yeye mwenyewe.Kuna wakati alikuwa anajua mambo kuliko walimu wake na hivyo akawa anapata shida katika masomo.Ameishi katika umaskini kwa miaka arobaini mpaka iq yake ilipoonekana kuvuka mipaka na akawa mmoja kati ya ma selebrity.






1.KIM UNG YONG.
Mtu huyu ana IQ ya 210 ambayo inasadikika kuwa ndio kubwa kuliko zote katika historia.Alianza kujifunza lugha mbalimbali akiwa na miaka mitatu.Alijifunza na kujua hesabu za kiwango cha advance akiwa na miaka minne na akapata OHD akiwa na miaka kumi na saba.


JE UNAFAHAMU KWAMBA HAWA NDIO WASANII WALIOSOMA PAMOJA NA SASA NI MAARUFU TANZANIA NA AFRICA

By // No comments:

HAWA NDIO WASANII WALIOSOMA NA KWENDA SHULE PAMOJA









Ommy dimpoz mzee wa nai nai na baadae amesoma na super producer Mensen Selkta akiwa amemtangulia kidato kimoko pale Mbezi High school
Mesen Selekta yeye ni producer kutoka de fetality records lakini pia ni msanii ambae keshatoa pini kama kushoto kulia, na nyamnyamu.
Jaffarai amesoma na Jay moe kuanzia darasa la pili mpka la saba katika shule ya msingi Makumbusho iliyoka kijitonyama Dar-es-salaam

Juma Mchopanga a.k.a Jay moe
Mangwea mzee wa freestyle amesoma shule moja na Mez B, Noorah na Daki Master katika secondary ya Mazengo iliyoka Dodoma 
Mez B
Daki master
Noorah
Bob jr ambae pini lake la Nichumu limekamata nafasi ya kwanza ndani ya Top20 za Clouds wiki hii, amesoma na producer Nah Real ambae ameshatengenez pini kama Pea ya Nikki wa pili na zinginezo katika shule ya msingi Olympio.
Mzee wa Ndehe mtini Feruz amesoma na jamaa wa Born Cruz waliowahi kutoa ngoma iliyofanya vizuri iayoitwa kaka poa(wanamuita kaka poa huyu jamaa, wanamuita mtoto wa watu huyu jamaa) katika shule ya sekondari ya Makongo
Ben paul amesoma na Baghdadi Azania Secondary, lakini Ben Paul akiwa A level na Baghdadi akiwa A level
Baghdadi
Msanii Suma Lee amesoma na Producer Duke kutoka M lab katiska shule ya sekondari Sahare iliyoko Tanga huku Suma akiwa mbele ya Duke ki madarasa
Mh Temba kutoka kiumeni amesoma shule na Solo Thang, Rich one, Chidi Benz, Soggy Doggy, marehem Kanumba na Dazz baba katika shule ya sekondary ya Jitegemee iliyoko Temeke, Dar es salaam
Sollo Thang
Chidi benz
Marehem Kanumba

MAUMIVU YA MGONGO,MKONO NA NJIA YA KUJIKINGA AU KUJITIBIA NA VYANZO PIA

By // No comments:

SPINAL DISC (DISC ZA UTI WA MGONGO)

ZINAVYOLETA MAJANGA



Spinal Disc ni disk zinazokaa kati kati ya pingili “Spinal Vertebrae” za uti wa mgongo. Kuna wakati disk hizo hutoka sehemu yake na kusogea pembeni tatizo ambalo linajulikana kwa majina kadhaa kama vile DEGENERATIVE DISC DISEASE au HERNIATED DISC au  SLIPPED DISC. Tatizo hili husababisha maumivu makali ya mguu, mgongo, bega au Mkono. Maumivu haya huwa ni makali mno, katika mazingira mengine huuja na kutoweka, katika mazingira mengine maumivu haya huwa endelevu.

Naamini wengi wetu tumeshawahi kusikia au kuona ndugu, rafiki, jamaa, jirani fulani akiumwa mguu, mkono, bega au mgongo tena kwa maumivu makali sana.

Wengi wamehangaika hospitali nyingi bila mafanikio, wengine wamekimbilia kwenye huduma za maombezi na wengine wamekimbilia kwenye tiba mbadala na wengine wamekimbilia kwa Sangoma.

Kote huko wamekosa ufumbuzi wengine wamepoteza maisha na wengine wamepata kupooza kabisa mguu au miguu wakiwa wameshatuoa fedha nyingi sana na mateso makali.





Nilibahatika kufanya mazungumzo na baadhi ya waliowahi kupatwa na matatizo kama haya. Ndugu Selemani Mkoba alinielezea tatizo hilo lilivyomtesa na baada ya kuhangaika hospitali kwa zaidi ya miezi 3 wakati wote kiteseka kwa maumivu makali na kupoteza hela nyingi bila mafanikio aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Anasema Mganga alimpa matumaini makubwa lakini wiki kadhaa zikawa zinapita bila kupata unafuu wowote. Anasema Mgonga alikuwa akimpa matumaini kwa kumwambia ugonjwa unaingia ghafla lakini kutoka unatoka taratibu sana . Ndugu Mkoba anasema kwa bahati alipomwelezea tatizo hilo mmoja wa rafiki zake ambaye si daktari alimwambia  aondoke haraka huko na kuwahi Muhimbili. Rafiki yake huyo alimweleza kuwa analifahamu tatizo hilo.

Ndugu Mkoba amasema alienda Muhimbili kama alivyoshauriwa na rafiki yake, akafanyiwa kipimo  cha MRI ambapo waligundua tatizo hilo katika uti wa mgongo na kupangiwa siku ya upasuaji. Alifanyiwa upasuaji na alipozinduka alikuwa na maumivu makali ya wastani yatokanayo na upasuaji tu .. maumivu ya mguu hayakuwepo tena. Maumivu yatokanayo na upasuaji yaliendelea kupungua na sasa ni miezi mitatu amebakiwa na maumivu madogo sana mbayo yanaendelea kupoteza huku akiendelea na mazoezi.  Anaweza kuendesha Gari, anaweza kutembea na kufanya shughuli zake ambazo zilisimama. Aidha Ndugu Mkoba anasema angependa watu wajue hili ili wasi mateso aliyoyapata yeye na walio kwenye mateso hayo wapate ufumbuzi haraka maana ni mateso yanayotisha.


MGAWANYIKO WA UTI WA MGONGO NA MATOKEO YA DISCK ZINAPOCHEZA

Uti wa mgongo umegawanyika katika aina kuu zipatazo nne (4) za pingili “Spinal Vertebrae”

Cervical Curve: Hili ni eneo la juu la uti wa mgongo, Eneo hili linaanzia uti wa mgongo unpokutana na kichwa na kuishia eneo la mwisho la Shingo, kwa lugha nyepesi ndilo eneo linalomiliki shingo, pingili zilizopo katika eneo hili zinaitwa “Cervical Vertebrae”.

·         Maeneo yanayoathiriwa na Disc kucheza katika eneo hili “Cervical Disc Herniation” ni Mikono au Mabega au kifua, moja wapo ya viungo hivi vitapata maumivu makali sana.

Thoracic Curve: Hili ni eneo la uti wa mgongo linalofuatia kuelekea chini likianzia inapoishia Shingo, Eneo hili linaishia katikati ya mgongo, kwa lugha nyepesi eneo hili ndilo linalomilike mbavu. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Thoracic Vertebrae”.

·         Kucheza kwa disck katika eneo hili kutakusababishia maumivu makali ya Mgongo eneo la juu ya Kiuno.

Lumbar Curve: Eneo hili linaanzia inapoishia Thoracic Curve na kuelekea chini na kukutana na Eneo linaloitwa Sacral Curve au eneo la kiuno linapoanzia. Eneo la Lumba linazungukwa na ma matumbo na mazagazaga mengine yasiyokuwa na mifupa. Pingili za uti wa mgongo zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Lumbar Vertebrae

·         Ikiwa Disc zitacheza katika eneo hili mhusika atapata maumivu makali ya mguu maumivu ambayo yaukumba mguuu wote kuanzia sehemu ya ndani ya tako na kushuka chini mpaka mwisho wa mguu kwenye kisigino.

  Sacral Curve: Eneo hili linaanzia pale Lumbar Curve inapoishia hadi mwisho wa uti wa mgongo kwa chini. Katika lugha nepesi eneo hili ndilo linalomiliki kiuno. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Sacral Vertebrae”

SABABU ZA MATATIZO HAYA

·         Ajali ya Gari
·         Kuanguka
·         Kupigwa/kupigana
·         Michezo
·         Ajali katika sehemu za kazi
·         Kasoro wakati wa kuzaliwa
·         Kubeba vitu vizito
·         Ukaaji mbaya wa muda mrefu
·         Misukosuku mbali mbali ya mwili kama

MATIBABU

Tatizo hili linatibika ikiwa mgonjwa atawahi kufanyiwa uchunguzi sahihi na tatizo hilo kugundulika.  Kuna matibabu ya namna tofauuti ambayo daktari anaweza kukupa lakini hali inapokuwa mbaya Madaktari hulazimika kufanya upasuaji. Mgonjwa anatakiwa kupimwa kwa vipimo sahihi na kipimo kinachoAMINIWA zaidi ni MRI. Aidha kwa bahati Tanzania moja ya nchi chache barani Afrika zenye mitambo hii ya MRI na moja ya nchi chache barani Afrika zenye madaktari bingwa wa matatizo haya.

Wadau  badala ya ya kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji tuwahi hospitali hususani Muhimbili kuonana na mabingwa wa NEURAL. Rai yangu kwa serikali pamoja na kuwa sisi tumekuwa moja katika nchi chache zenye huduma hii, mahitaji ya Madaktari hawa ni makubwa sana bado, Serikali ipeleke Madaktari zaidi nje kwa ajili ya kupatiwa ujuzi huu na kuongeza mashine za MRI angalau zifike 10.

NAMNA YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI

Matunzo mazuri ya ujauzito
Kuepuka kipigana au kupigwa, usimpige mwenzako kwasababu unaweza kumsababishia tatizo baadae
Kama unaendesha gari ama piki piki kuepuka mwendo unaoweza kukusababishia ajaili
Uangalifu katika michezo na mazoezi mazito
Kujilinda kiafya ili kujiepusha na maradhi yasiyotambulika
Tujiepusha na ukaaji mbaya wa muda mrefu katika sehemu zetu za kazi, pendelea kutafuta maelekezo jinsi ya kukaa katika sehemu yako ya kazi.
Pendelea kuangalia afya mara kwa mara na kupata ushauri wa madaktari

A REAL EDUCATED AND INSPIRING DOCTOR ...YES DOCTOR BEN CARSON TALKING ABOUT LEADERSHIP

By // No comments:

WATCH TO KNOW HOW YOU CAN PASS EXAMS

By // No comments:

NJIA ZA KUZUIA NA KUONDOA CHUNUSI USONI

By // No comments:

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .



Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.


Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.


Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.


Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.

Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.


Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.


CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;


1. UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi


2. VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.


3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
4. DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.


5. MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.


6. MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.


7. JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.


8. FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.


9. HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.

10. USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi


11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi

DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana

Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi


MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.
Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.


DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.
Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.

Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.


DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na
”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”


Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.


MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.

MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.


Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi


MUHIMU
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.


MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
1. Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.


2. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando

3. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)


4. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.


5. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.


6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D


7. Punguza mawazo
.....pole kwa tatizo hili na matumain yangu ukifuata njia hizi zote kwa ufasaha utafanikiwa .KIKOTI

JINSI ELIMU ITAKAVYOKUKWAMUA KATIKA MAISHA NA KUWA NA MAFANIKIO

By // No comments:

Hali ya uchumi duniani imekuwa ngumu si hapa kwetu Tanzania tu bali pia hata katika nchi zilizoendelea. Uwezo wa serikali nyingi duniani hasa wa kutoa huduma kwa watu wake unazidi kupungua kutokana na serikali nyingi kuelemewa na madeni. Matatizo yaliyosababisha hali hii ni pamoja na; kushuka kwa thamani ya pesa, kupanda kwa deni la taifa, ongezeko la watu, kupanda kwa bei ya mafuta,makampuni kufilisika na wafanyakazi kupunguzwa kazini na kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali kwa jamii. Hali hii inazidi kuwagusa watu wengi zaidi duniani pengo la masikini na matajiri linazidi kuwa kubwa na tabaka la kati linaanza kutoweka. Hali hii ikiendelea kama ilivyo kutakuwa na matabaka mawili tu duniani yaani matajiri na masikini.  Jee unawezaje kuepuka kuingia katika tabaka la umasikini na kuingia katika tabaka la matajiri? Suluhisho ni kuwa mjasiriamali kwa kujifunza na kutekeleza kwa vitendo mbinu za ujasiriamali.

Watu wengine wamekuwa na dhana potofu kwamba tatizo la umasikini linatokana na ukosefu wa pesa au mitaji peke yake lakini mimi ninamtizamo tofauti, kama tatizo la umasikini lingekuwa ni ukosefu wa fedha kuna matajiri wawili kule Marekani, Donald Trump na Robert Kiyosaki wamesema kwamba wangejitolea kuwagawia watu pesa lakini katika utafiti wao wamegundua kwamba hata ukimpa mtu pesa atatumia zikiisha atarudi tena kuja kuomba, hivyo mbinu hiyo siyo endelevu inamfanya huyu anayeomba kuwa tegemezi na kuzidi kuwa masikini. Kwa hiyo walichukua msemo wa kichina kwamba ukitaka kumsaidia mtu uasimpe samaki ila umpe nyavu na mbinu za kuvua samaki. Vivyo hivyo katika kumkomboa mtu kutoka kwenye umasikini unatakiwa kupatia elimu ya ujasiriamali na namna ya kutumia mbinu hizo.  Kwa hiyo watu hawa pamoja na wanaharakati wengine wa kupambana na umasikini tumeamua kutoa elimu ya ujasiriamali kwa kutumia njia mbali mbali. Kwa maoni yetu pesa haikufanyi wewe kuwa tajiri bali elimu ya ujasiriamali ndiyo inayoweza kukufanya kuwa tajiri. Kama pesa ingekuwa inao uwezo wa kuwafanya watu wawe matajiri kuna mifano mingi tu ya watu ambao walipata bahatinasibu ya mamilioni na wastaafu ambao walipata mafao ya mamilioni ya fedha lakini kwa kukosa elimu ya ujasiriamali wametumia pesa zote na kufilisika.

Kila mtu ana matatizo yake ya kifedha  katika dunia ya sasa kuwa na elimu na kuwa na Shahada ya fani fulani pekee haitoshi unatakiwa kuwa na elimu pia ya ujasiriamali, kutegemea pensheni peke yake ni tatizo, kwani utafiti uliofanyika ni kwamba Wastaafu wengi ambao wanategemea pensheni zao huishiwa ndani ya miaka 5 baada ya kustaafu na kulipwa mafao yao ya mkupuo na zile hela za pesheni wanazolipwa  kidogo kidogo kila mwezi  huwa hazitoshi hata kukidhi mahitaji ya muhimu ya watu hao na kuwafanya waishi katika hali ya umasikini. Sizungumzii hali hii kwa nia ya kuwatisha watu  ila hii ndiyo hali halisi kama ukitaka kuthibitisha maneno haya waulize wazee wastaafu watakwambia kuhusu taabu wanazozipata.

 Watu wengine wamekuwa na mawazo ya kuitegemea serikali iwakwamue katika matatizo yao ya kifedha hayo pia ni mawazo potofu. Serikali haiwezi kukutatulia matatizo yako ya kifedha ila ni wewe mwenyewe ndiyo unaweza kutatua matatizo yako ya kifedha kwa kuchukua hatua kupata maarifa ya ujasiriamali, kubuni shughuli za uzalishaji mali utoaji huduma na biashara.  Bahati mbaya hata wajasiriamali tulionao wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa mazoea hivyo kuzifanya zisiwe endelevu. Kama wewe ni mjasiriamali wekeza kwenye maarifa ya ujasiriamali pia ili uinue hali yako ya maisha. Unaweza kujiendeleza kwa kusoma vitabu vya ujasiriamali, kusoma makala kama hizi kwenye magazeti, kuhudhuria mafunzo na semina za ujasiriamali ambazo huwa zinatolewa na watu mbali mbali.

Mtaji mkubwa uliopewa na mwenyezi Mungu ni akili yako. Watu wengi hatutumii vizuri akili zetu katka kufikiria namna ya kutatua matatizo yetu, kwa mfano unapopata tatizo lolote badala ya kufikiria kuhusu tatizo hilo anza kufikiria namna ya kutatua tatizo hilo. Pia kama ukimudu kufikiria namna ya  kutatua matatizo yako basi unaweza kuanza kufikiria namna ya kutatua matatizo katika jamii ukisha jua matatizo yanayoikabili jamii unaweza kutafuta suluhisho na hilo suluhisho unaweza kulifanya likawa fursa ya biashara. Kwa mfano kuna mtu mmoja alikuwa anaishi katika kijiji kimoja katika kutafuta mahitaji yake ya kila siku kama vile sukari, majani ya chai unga wangano nk. alilazimuka kutembea umbali wa kilomita 3 kila mara ili kwenda kununua mahitaji yake kijiji cha jirani. Alivyochunguza akagundua kwamba tatizo hili lilikuwa si la kwake peke yake hata wanakijiji wenzake walikuwa wakihangaika kufuata bidhaa hizo kijiji cha jirani kama yeye ndipo hapo jamaa aliamua kuanzisha duka la rejareja katika kijiji chake, na kwa kweli duka lake liliendelea sana na alipata pesa nyingi.   Ili ufanikiwe kiuchumi maishani unapaswa kuwa mtundu, mbunifu na mtafiti.

Eneo lingine ambalo hatulitumii ni kukagua vipaji vyetu. Mwenyezi Mungu kamjalia kila mtu kipaji chake, wengine ni waimbaji wazuri, wasusi, wasanii, wachekeshaji, washereheshaji, wakimbiaji, wapishi wazuri nk. Jee umewahi kijuliza una kipaji gani? Kama hujui waulize watu wako wa karibu, kama vile baba, mama, kaka, dada, rafiki, mke mume nk. Jee unakitumia kipaji chako ipasavyo kukuletea maendeleo yako kiuchumi? Kwa mfano kama wewe ni msusi mzuri kwa nini usianzishe saluni? Kama wewe una kipaji cha kupika kwa nini usianzishe hoteli? Bahati nzuri sana kipaji chako kinaweza kuwa ndiyo mtaji wako mkuu wa kuendesha biashara yako. Muhimu ukigundua kipaji chako lazima ukiendeleze.

Jee unapaswa kufanya nini ili upambane na tatizo hili la umasikini? Kwanza unapaswa kuwa na shuguli ya kufanya. Inasikitisha kuona watu wazima wanakaa vijiweni, kina babu wanashinda kwenye kahawa na kucheza bao siku nzima au vijana wanacheza pool siku  nzima. Mtu yeyote aliyefikisha umri wa miaka 18 anapaswa kuwa na shughuli ya kufanya kama ni ya kuajiriwa au ya kujiajiri. Jee wewe ni kati ya  watu wengi ambao  wana mitaji lakini hawajui wafanye nini unaweza kutumia akili yako kubuni shughuli ya kufanya au kutumia kipaji chako kufanya biashara. Hatua ya pili ni kujenga tabia ya kuweka akiba. Katika dunia ya sasa kuna sehemu nyingi ambazo unaweza kuweka akiba yako mfano kwernye SACCOS, akaunti za akiba kwenye benki mbali mbali. Unapaswa kuweka kati ya asilimia 10 % hadi 15 % ya mapato yako kwa mwezi. Mwisho ni kuwekeza fedha zako katika vitegauchumi endelevu. Jee ni vitegauchumi gani ambavyo ni endelevu, kuwekeza katika majengo ya kupangisha. Kwa nini tunashauri uwekeze pesa zako katika vitegauchumi ni kwa sababu pesa ikikaa sana benki huwa inaongezeka kidogo kidogo kwani faida inayopatikana ni ndogo kuliko mfumuko wa bei hivyo baada ya muda pesa yako itashuka thamani, lakini ukiwekeza kwenye kitegauchumi endelevu thamani ya pesa yako inapanda. Kwa mfano ukiwekeza kwenye majengo ya kupangisha kila hali ya uchumi inavyozidi kuwa mbaya thamani ya majengo na kodi ya nyumba inapanda.Vitegauchumi huingiza pesa bila kukulazimu kuendelea kufanya kazi hivyo hata ukizeeka au kuugua au kufukuzwa kazi vitegauchumi vyako vinaweza kukulinda kwani vitaendelea kukupa kuipato bila kufanya kazi. Swali la kujiuliza ni jee chanzo chako kikuu cha mapato yako ni katika kazi unazozifanya kila siku au kutoka kwenye vitegauchumi? Kama unategemea kazi kuingiza sehemu kubwa ya kipato chako una hatari ya siku moja kurudi kwenye umasikini kama ukiugua muda mrefu, kufukuzwa kazi au kustaafu.Jitahidi kuwekeza pesa zako kwenye vitegauchumi vilivyo endelevu ili uwe na uhakika wa maisha.
Mr.Kikoti. Powered by Blogger.

Comments