FAHAMU FAIDA NA HASARA ZA KUJICHUA{PUNYETO}

By // No comments:
SOCIAL HALL
SOCIAL HALL
 

Punyeto  Ni nini?
Kufanya au kupiga punyeto,  ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.


Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine. 


Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha. 


Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.


Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe. 


Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi. 


Unaweza kufikia kilele cha starehe yako
(kwa wanaume) kwa kutomasa tomasa uume au (wanawake) uke, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako. 

kwa kawaida au mazoea ni kuwa punyeto huwa inafanywa na vijana wa umri wa kubalehe au kuvunja ungo na hii ni kwamba mwili unakuwa unapokea mabadiliko hasa maumbile, sauti,vipele usoni hapo kijana anakuwa na shauku ya tamaa za kimwili ,wakati huo kijana anakuwa hana mwenza kwa hiyo inawalazimu kujilizisha kimwili..

Lakini hata watu walio katika mahusiano pia wanapiga punyeto ingawa si kwa kiasi kikubwa kama kwa vijana wanaoanza kubalehe

KWA NINI PUNYETO HUONEKANA KUWA MAKOSA? Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa.

Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.

Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine.

Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto.

FAIDA ZA KUPIGA PUNYETO.
1 . Kuujua mwili wako na kujiamini zaidi linapokuja swala la kungonoka (fanya mapenzi)
2 . Kuongezeka kwa hamu ya kufanya mapenzi kwa vile utakuwa unajua utamu wake.
3.  Kujua "vipele vyako viliko".
4.  Kutokuusaulisha mwili wako ikiwa uko nje ya uhusiano au umeamua kuwa single kwa 
     muda.
5.  Kuepuka mimba na maambukizo ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine    

     yanayotokana na ngono zembe. 

Hizi ni baadhi tu ya faida zipo faida nyingi. MADHARA YA KUPIGA PUNYETO. Ifahamike kuwa kuna watu wengi sana wanatumia mikono yao kujisaga katika sehemu nyeti, Jambo hili linamadhara makubwa sana kwa binaadamu, Jambo hili kwa lugha ya kiingereza wanaliita Masturbation (
Manual erotic stimulation of the genitals or other erotic regions, often to orgasm, either by oneself or a partner.) ni kitendo cha mwanaume kujisugua uume wake.

Licha ya tafsiri ya punyeto kuwalenga wanaume zaidi lakini kuna Usagaji na madhara yake kwani hili linahusu wanawake na hili la usagaji linaingizwa na punyeto kwani madhara yake yanakaribiana lakini tofauti inakuja jinsi ya kujirizisha.

Wanaume wengi sana wanatumia mikono mikavu kujisaga, jambo hili huwafanya waharibu mishipa ya fahamu inayounganisha uume na mfumo uliopo kwenye ubongo
. Uharibifu huu humfanya mwanaume apoteze msisimko wa kujamiiana au hata akiupata humfanya ashidwe kufikisha hisia zake kisawasawa hasa akikutana na mwenza wake ambaye sehemu zake nyeti ni laini sana tofauti na mikono alozoea kujichua nayo.

Jambo jingine hatari linalo mkabili mpiga Punyeto ni upotevu wa hisia wakati wa kujichua kwa mfano ili afike kwenye kilele lazima akuze hisia zake kwa kiwango cha juu, pengine kupita ukweli halisi ataokutana nao pindi atakapokuwa na mwanamke faraghani.

Mpiga Punyeto hajitoshelezi mpaka amlete kwenye hisia mrembo zaidi (anayemjua au alimuona sehem akampenda) kisha amvike utundu wa kimahaba ampe manjonjo hadi mwenyewe atosheke, kwa namna hii mwanaume mwenye kufanya mazoea ya kufanya hisia za wanawake warembo ambao hawezi kuwapata kwa hali halisi anapokutana na kina Mwafulani wa mtaani tena sio mtundu kimapenzi, hapo kamwe hawezi kusisimka mwili na hivyo kujikuta Uume wake husimama kwa kiwango cha chini sana.

Madhara mengine yanayopatikana ndani ya kitendo hiki ni kuumwa kichwa, mgongo, kupoteza nguvu za mwili na macho, madhara mengine makubwa hasa mwanamme anaejichua mara mbili au tatu kwa siku ni kushindwa kuzalisha, hii inatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume kwenye mfuko wa uzazi.

     Hii yote madhara ya hapa duniani lakini kwa MUNGU amesema  

''Amelaaniwa mtumiaji mkono kwa kujisugua uume wake (Punyeto)
Kujichua kwa kutumia sanamu kunaweza sababisha kulegea(kutepeta) kwa nyama za nyeti zako(inategemea na aina ya sanamu), kupoteza hisia za uume halisi kutokana na kuzoea dubwana hizo, kifo kutokana na mshituko ikiwa unatumia ya umeme, vilevile saratani ikiwa unatumia vilainishio ili kurahisisha hilo sanamu kuingia.


ZINGATIA: -
kujichua kupita kiasi kunaweza kusababisha kupoteza hisia halisi ya uume

JINSI YA KUFANYA MENO YAKO KUWA MEUPE NA YA KUPENDEZAA

By // No comments:
JINSI YA KUFANYA MENO KUWA MEUPESOCIAL HALL
SOCIAL HALL




Wakati wa muongo uliopita mahitaji ya kuboresha muonekano au kurembesha meno yameongezeka kwa kiwango kikubwa hasa katika nchi zilizoendelea. Hii imechochewa na kupatikana kemikali mpya za meno (dental

meterials) na vifaa kwa kasi ikiendana na kuboresha vile vya zamani. Sehemu nyingine iliyosababisha madaktari na mainjinia wa meno kuyafanya meno kuwa meupe ni sehemu ya fani ya taaluma ya meno chini ya urembeshaji wa meno, fani hii uhusika na kuboresha muonekano wa meno hasa yale yanayoonekana wakati

wa kutabasamu na kuongea. Inahusisha matibabu kama kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe, kunyoosha meno yaliyojipanga vibaya pamoja na kukarabati meno yaliyovunjika na yale yaliyoumbika visivyo (malformed teeth). Huko Uingereza na sehemu nyingine za magharibi wanawake walio wengi wanatumia maelfu ya paundi/euro kuboresha muonekano wa meno yao hali ambayo inaanza pia kuingia huku kwetu.

Nini husababisha meno kugeuka rangi?
Meno kugeuka rangi husababishwa na kimojwapo au muunganiko wa vitu vifutavyo: -


Vyakula na vinywaji kama vile vinyaji vyenye kaboni, wine na sigara.
Utumiaji wa maji yenye kiwango cha juu cha madini aina ya magadi (fluoride) na utumiaji wa magadi katika kulainisha vyakula wakati wa kuandaa vyakula vigumu kama maharage na makande. Utafiti uliofanywa na Prof.

Mabelya na wenzake nchini Tanzania umeonesha kuwa kubadilika kwa rangi ya meno kutokana na magadi kwa kiwango kikubwa husababishwa na matumizi ya magadi katika mapishi ya vyakula hasa makande kule maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro/Moshi kuliko inavosababishwa na matumizi ya maji.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ngumu za jino (enamel and dentine defects). Iwapo sehemu ngumu ya meno imeumbwa ikiwa laini ni rahisi kufyonza rangi na jino kuota likiwa limegeuka rangi au kubadilika baada ya kuota.

Matumizi ya madawa kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayajapata madini ya kutosha na hata watoto wachanga ambao meno yao hayajakomaa.
Kufa kwa kiini cha jino hasa kutoka na kujigonga wakati wa ajali au kupigana ngumi usoni (pulp necrosis), jino

likigongwa kwa nguvu damu huvuja ndani ya kiini cha jino na baadaye huchachuliwa na kutoa kemikali ambayo hupenya kwenye vitundu vidogo vidogo kwenye dentine na kujidhihirisha kama kijivu, zambarau au hata

nyeusi. Hali hii yaweza tokea mapema baada ya kupata ajali lakini wakati mwingine inaweza kuchukua miaka kadhaa hata arobaini kipindi ambapo mtu hakumbuki kuwa aliwahi kutwangwa ngumi.
Kuyafanya meno yenye rangi yasiyompendeza mwenye nayo kuwa meupe
(Bleaching or teeth whitening)

SOCIAL HALL


 Huku ni kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe au kuongeza weupe wa yale yenye rangi ya kawaida kufikia kiwango cha weupe atakacho muhitaji kwa kutumia kemikali maalum. Rangi ya kawaida ya meno kwa walio wengi ni uweupe kama wa maziwa (milky white). Rangi yeyote nje ya hiyo si ya kawaida (abnormal color or discoloration).


Kuwa na rangi isiyo ya kwaida hasa kwa meno ya mbele linaweza kuwa tatizo kubwa la urembo na kumsumbua mhusika kisaikolojia. Kuyafanya meno kuwa meupe kumelenga kuwaondolea wahusika tatizo hili japo mafanikio yake yanategemea kiwango cha rangi isiyo ya kawaida.


Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia kemikali, kunaweza kubadili yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kutoka yale yaliyoathirika kwa kiwango kidogo mpaka cha kati.


Kufanya meno yawe meupe kwa kutumia kemikali huunguza (oxidises) rangi ya jino na kuiondoa. Kemikali zinazotumika zina hydrogen peroxide 30%-35% na baadhi carbamide peroxide 10%. Kemikali hizi huweza kuondoa rangi zilizosababishwa na vyakula, vinywaji, dawa za tetracycline, rangi kidogo iliyotokana na utumiaji

wa madini ya magadi kwenye vyakula au kwenye maji (mild fluorosis) na meno yenye rangi ya njano au kijivu itokanayo na umri kuwa mkubwa. Inaweza pia kuondoa rangi itokanayo na uvutaji wa sigara na matumizi ya ugoro. Kwa wavutaji wa sigara sharti waache pindi watumiapo kemikali hizi kwani muunganiko wa hydrogen

peroxide na kemikali zilizopo kwenye moshi wa sigara unahisiwa kuongeza madhara zaidi ambayo tayari moshi wa sigara husababisha kwenye mwili wa binadamu. Haishauriwi kwa akina mama wanaonyonyesha kutumia dawa hizi pamoja na kwamba hakuna madhara yanayojulikana mpaka sasa.


Kuboresha weupe kwa kutumia chemikali

Kupiga meno viraka (Veneering)
Hii hufanyika kwa kuondoa sehemu ndogo ya juu ya jino kwenye enamel kama 0.5-1mm na baadaye kupandika dawa yenye rangi nyeupe kulingana na mgonjwa anavyotaka mwenyewe. Picha inayonesha meno yaliyobadlika rangi kutokana na magadi kabla na baada ya kupigwa viraka


Kabla ya kiraka. Na Baada ya kupigwa kiraka(veneer)

Kumbuka: kuna rangi zaidi ya 26 nyeupe ambazo miongoni mwake mgonjwa anaweza kuchagua anayoitaka..SOCIAL HALL

MAPENZI NI NINI??? FAHAMU SASAMAJIBU YA SWALI LAKO

By // No comments:
  1. 
    MAPENZI NI NINI???
  2. SOCIAL HALL
    SOCIAL HALL

     
    
    Upendo umetokana na neno la kigiriki “ahab aheb” lenye maana hisia kali na muhathirika wa ndani. Upendo ni hisia kali, upendo chimbuko lake ni moyoni upendo ni Mungu ameuweka ndani ya moyo wa mwanadamu, upendo ni maisha ya mtu na ni utaratibu wa mtu hivyo mtu anapo amua kumpenda mtu mwingine mtu huyu anakua ameamua kuhatarisha maisha yake kwa mtu Fulani. Ameamua kuuweka moyo wake kwa mtu Fulani. Ameathirika ndani ya moyo wake kwa ajili ya mtu Fulani akili ambayo ndio chanzo cha mapenzi imekubaliana nayo. Najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni akili,kama akili ikichoka hakuna mapenzi hivyo ndio maana hata maandiko yanasema “ Ishini na wake zenu kwa akili”
     
    Maana mapenzi la kweli yanahitaji akili timamu uwe na muda wa kufikiri kabla ujafanya lolote. Kuishi na mtu kunahitaji akili timamu, sasa mtu huyu amefanya maamuzi ya kiakili, kimwili na kiroho kuwa wewe unamfaa hivyo unatakiwa kuyaheshimu na kuyadhamini mawazo yake na kuyatendea kazi kwa uangalifu sana UPENDO NI MSUKUMO WA NDANI YA MTU.
    Upendo si kitu cha kuchezea mpendwa mwenzangu. Upendo ni uhai wa mtu. Ndiyo maana maandiko yanasema: “Upendo una nguvu kuliko mauti”
    Hili andiko wewe unalielewaje? Mimi ninavyolielewa ni kuwa Upendo ni zaidi ya kifo yaani Upendo ni heri kuchagua kifo kuliko kuchagua kupenda au kupendwa maana upendo umekamata moyo na wewe unaelewa kazi ya moyo kwa mtu? HEART – kwa kiyunani ni (leb) – mind ni ufahamu, midst (labab) Kiyunani – inner person – yenye maana ya undani wa mtu – mind and heart – which also includes decision making ability- (ufahamu na moyo ambayo hujumuishwa pia maamuzi yanaweza kufanyika (Mwanzo 6:5-6) vilevile moyo unasimama kama (kiungo cha mwili) 2Sam 18:14- can be used of the innerman- undani wa mtu unaweza kutumika hivyo.
    Moyo unakuwa kama – hisia (emotions Kumb 6:5) moyo – furaha waamuzi 16:25
    Moyo una hofu na huzuni ISam 24:10
    Moyo unaweza kujaribiwa zab 86:11
    Moyo unaweza ukawa mgumu wakati mwngine kumb 30:6
    Hivyo maumivu ya moyo sio mchezo, haya ni maumivu ya ndani kwa ndani. Maumivu yake yanatembea ndani ya damu haya ni mateso makubwa sana maana unaweza ukawa umelala mwili lakini nafsi hailali inahangaika usiku kucha – unauwezo mkubwa wa kwenda kulaa umechaka na kuamka umechoka maana nafsi ilikuwa inatafuta.

    a) kufarijiwa kutiwa moyo,
    b) upendo kudhaminiwa,
    c) kuheshimiwa,
    d) kukubalika,
    e) kutambulika na mtu anayefaa maana upendo hautafuti watu bali unatafuta mtu haijalishi awe amesoma, hajasoma, tajiri au masikini, mweupe au mweusi, mfupi ama mrefu Upendo unamtafuta mtu (a person)
    Moyo – ndio eneo ambalo maamuzi yenye nguvu yanafanyika – kuaminiana ndio maana hata maandiko Matakatifu yanasema “Mtu moyoni huamini na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu” na andiko lingine linasema
    “Watu hawa wananiheshimu kwa midomo tu lakini mioyoni mwao wako mbali nami”
    Hivyo upendo wa kweli huanzia moyoni. Unaamini tokea moyoni kuwa huyu ndiyo, anayenifaa katika moyo wangu, unamdhamisha tokea moyoni mwako anakuwa na kibari kikubwa maishani mwako kuwa huyu ndiye kisha kwa kinywa unamdhibitisha kuwa ndiye.

    PENZI LA KWELI LINAONGEA MOYONI.
    1. Moyo huthibitisha kuwa huyu ndio anayenifaa maishani mwangu.
    2. Aliyepata kibali moyoni mwangu.
    3. Ndiye niliyemtafuta usiku na mchana.
    4. Aliyeutesa moyo wangu.
    5. Aliyeuyumbisha moyo wangu mara tu nilipomwaona.
    6. Mwenye uwezo wa kutimiliza ndoto yangu.
    7. Kioo cha maisha yangu.
    8. Faraja wa moyo wangu.
    9. Huyu ndiyo mwandani wangu (msiri)
    10. Kitambulisho cha maisha yangu.
    11. Mbeba maono yangu.
    12. Heshima yangu katika jamii itakayo nizunguka.
    13. Mtetezi wangu asiyeweza kuvumilia nisipate aibu katika jamii.
    14. Mfuta machozi na majasho yangu.
    15. Mratibu wa moyo wangu.
    16. Chemichemi ya furaha yangu.
    17. Barafu wa moyo wangu.
    18. Asali wa moyo wangu.
    19. Malkia na Mfalme wa moyo wangu.
    20. Chanzo cha afya yangu.
    21. Mjenzi wa familia yangu.
    22. Mwalimu wa familia yangu.
    23. Mlinzi wa ndoto na maono yangu.
    24. Adui wa adui zangu.
    25. Mponyaji wa majeraha yangu yaani doctor wa moyo wangu.
    26. Rafiki wa moyo wangu.
    27. Ngao ya moyo wangu.
    28. Ufunguo wa maisha yangu.
    29. Ua la moyo wangu.
    Huyu ndiye mpenzi anayetafutwa na mtu yoyote katika Dunia hii ya leo mwenye sifa hizi mpendwa, mapenzi yana nguvu sana kuliko unavyodhania kuna watu walikosea katika kuchagua leo wanalia usiku na mchana ndoa imekuwa ndoano mapenzi yamevamiwa na shubiri, moto umewaka matusi, dharau, kiburi, jeuri, ngumi ndio yamechukua maisha kweli mapenzi yanatesa moyo, yanaumiza, yana katisha tamaa, yana poteza maana ya mtu, yanavuta mauti ukiyakosea utanielewa ninamaanisha nini? –MOYO ndio chanzo cha furaha – ukichafuliwa furaha hukimbia na amani, hapo ndipo hofu inapochukua nafasi unajikuta unaanza kumuogopa mpenzi wako, na wakati upendo wa kweli hauna hofu hata kama mke au mume ni mkali namna gani Upendo wa kweli huondoa hofu lakini ukiona mtu anamuogopa mwenzi wake hapo tambuakuwa penzi hilo limevamiwa na adui, moyo umepoteza dira umekosa matumaini na huyo uliyenaye, Hofu huvuta dhambi hapo ndipo unapoweza kuona mtu anatafuta rafiki mwingine ili aweze kumlinda kumrudishia amani yake, kumponya majeraha yake hapo sio mchezo inabidi unapotambua hivyo unatakiwa kutengeneza maana hapo ndio chanzo cha magonjwa, talaka n.k fanya kwa bidii kujiaminisha katika moyo wa mwenzi wako ili mambo yasiharibike
    Moyo ukiumizwa HUZUNI hutokea hapo ndipo maombolezo yanapoanza, mtu huyu utamkuta analia kila unapomuona na machozi yanamdondoka,
    [a] moyo wake unalia.
    [b] Moyo wake unatoa damu kidonda kibichi.
    [c] Maombolezoyaliyo beba majuto kwa nini nilikubali kuwa na huyu?
    [d] Kama ningelijua nisingekubali.
    [e] Alitokea wapi huyu, Ee Mungu mbona ulimruhusu huyu mtu kuchukua moyo wangu najuta kukutana naye
    [F] Amepoteza furaha ya moyo wangu, ameharibu udhamani wa maisha yangu, msambaratishaji wa ndoto yangu.
    [g] Adui wa maisha yangu mpinzani wa maendeleo yangu.
    Haya maombolezo yanapozidi kuendelea mtu huyu anaamua kufanya maamuzi ambayo wengi hawataweza kukubaliana nayo, ila yupo kwenye harakati ya kujiokoa nafsi yake hata kufikia kuchukia kupenda au kupendwa maana teso alilopata ni kubwa sana wewe usifanye unajua sana kuongea hujui teso la mapenzi hujui moyo wa mtu ulivyoumizwa – usidanganyike na muonekano wake – aliyeumia yupo.
    Unaweza kumuona amelala kitandani na wakati mtu wa ndani amekaa kwenye mkeka anamsiba mkubwa,
    [a] Machozi hayamuishi
    [b] Mawazo yamemsonga sana,
    ]c] Moyo umesafiri haupo pale,
    [d] Kazi haziendi,
    [e] Huduma yake inazidi kuharibika kila siku,
    [f] Afya inakwisha kila siku,
    [g] Ofisini haonekani kazini anakuja lakini nafsi yake haipo pale na hata wengine wanaweza kutambua kuwa mwenzetu hayupo hapa.
    Unaweza kuongea na mtu ambaye nafsi yake ipo nyumbani kwake sio mchezo. Hapo ndio chanzo cha Msongo wa mawazo hutokea, moyo ulioumizwa kimapenzi unahitaji uangalifu sana kuutibu na kuushauri. Wachungaji wengi wamechangia ndoa za wengi kuvunjika kwa kutokuwa na ufahamu mkubwa wa upendo na matokeo yake, usiwe mwepesi wa kutoa maandiko mengi wakati hujui mateso ya mapenzi najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni sumu, yanapoharibika hutakiwi kuwa mwepesi kuyaingilia maana mapenzi yamebeba maisha ya mtu,
    Unapotaka kumshauri mtu aliyeathirika na mapenzi unatakiwa kuyafahamu mambo haya muhimu nayo ni:-
    1. Unatakiwa kujua maana ya upendo na gharama zake.
    2. Lazima ujue vyanzo vya kujenga uhusiano ili uwe imara na mwenye nguvu katika maisha ya wapendanao.
    3. Mambo 32 yanayojenga uhusiano kama ulivyosoma.
    4. Lazimaujue mambo yanayoweza kuharibu mahusiano na milango ya kuvunja mahusiano.
    5. Lazima ujue maumivu ya mapenzi ili uweze kuwaponya waliojeruhika kimapenzi.
    Nina maswali ya kujiuliza kuhusu UPENDO jambo hili ni kubwa sana katika maisha ya mwanadamu hakuna asiyejua maana limechukua sehemu kubwa katika MOYO wa mwanadamu,watu wengi tumekuwa tunalia sana, tumekuwa tunakata tamaa,tumekuwa tukigombana, hata hatua ya kuumizana na wengi wamekufa na wengi hawataki kupenda tena. Na kundi lingine linasema kupenda ni mzuri sana wanasema unanguvu sana na wakati mwingine wanasema kupenda ni kifo na wanaona unakupeleka jehanamu katika sehemu saba zifuatazo:
    1. Sehemu ya mateso
    2. Sehemu ya mahangaiko
    3. Sehemu ya masikitiko
    4. Sehemu ya magomvi
    5. Sehemu ya matukano
    6. Sehemu ya kudhalilishwa
    7. Sehemu ya kuchafuliwa
    Kwa nini tunapenda na kwa nini tunatumia ikiwa upendo ni mzuri Ni nani anayesababisha nipende na ninanianyenipenda kweli? Ni ninani nitayempenda? Na kwanini upendu unanguvu na imechukua sehemu kubwa ya maisha yangu? Sasa upendo ni nini na inamaana gani?

    ZIPO AINA SITA [6] ZA MAPENZI(UPENDO)
    1. Philotheos - upendo wa mungu; 2timoth 3:4
    2. Philoxenos - kupenda wageni [ xenia…..hospitality
    3. Philagathos - kupenda kitu kizuri; titus 1:8
    4. Philarguros - kupenda pesa; luke 16:14 and 2timoth 3:2
    5. Philautos - kumpenda mtu mmoja; 2timoth 3:2
    6. Philedonos - kupenda starehe; 2timoth 3:4
    Unajua ni vizuri sana kama utapenda mahali unapopendwa kuliko kupenda mahali usipopendwa, unatakiwa uwe na ufahamu mkubwa sana wa mapenzi kabla ya kuyaingia unaweza kupoteza ndoto zako za maisha, maaana mapenzi yanauwezo mkubwa sana wa kuharibu maisha yako. Mabinti wengi na vijana wamejikuta wameingia katika mchezo huu wa mapenzi wakiwa na akili za kitoto huku wakijua kuwa upendo ni kitu cha kawaida leo wanalia sana kutokana na maumivu waliyoyapata. Rafiki yangu ningependa nikwambie Upendo ni nini ?
    1. Upendo ni mzuri sana kama utajua maana na kusudi la Mungu kuweka pendo ndani ya mtu.
    2. Upendo unatesa
    3. Upendo unaua
    4. Upendo unakondesha
    5. Upendo unaharibu maisha
    6. Upendo unaharibu utaratibu wa mtu
    7. Upendo unanyonga maisha
    8. Upendo unaathiri akili ya mtu
    9. Upendo ni gharama
    10. Upendo ni shule
    11. Upendo ni maisha ya mtu.
    Mpendwa wangu neno hili (Upendo) sio kitu cha mchezo, wewe unaweza kuwa ni mtoto, mwanafunzi hujajipanga bado utaratibu wako wa maisha unatakiwa uwe makini sana katika jambo hili, unajua kuwa Upendo unauwezo mkubwa sana wa kutoa ufahamu wa mtu na kuharibu utaratibu wa mtu? Upendo unapoingia ndani ya moyo mtu anauwezo mkubwa wa kukutoa katika mipango yako, upendo ukikolea watu wanauwezo wa kusahau familia zao, masomo, kazi zao, na utaratibu wake wa kila siku unaharibika, upendo unatakiwa kuheshimika na kila mtu unatakiwa kutembea katika upendo kwa unyenyekevu mkubwa, utiifu na adabu maana sio jambo la mchezo, usichukulie jambo hili kitoto unatakiwa unapoamua kufanya maamuzi ya kupenda au kupendwa unatakiwa uwe na maswali (14) hayo ya msingi ili usije kuumia kama sisi tulivyoumiza na kuumizwa bila kujua, maana yake na gharama yake.
    MASWALI KUMI NA NNE(14) YA KUJIULIZA KABLA YA KUCHUKUA UAMUZI WA KUPENDA AU KUPEDWA
    1. Kwa nini ninapenda?
    2. Upendo ni nini?
    3. Je huyu anayenipenda anajua maana ya kupenda?
    4. Je amenipendea nini?
    5. Je ana malengo gani juu ya maisha yangu?
    6. Amejipanga vipi juu ya makwazo yatakavyo jitokeza baadaye?
    7. Je amenipenda love au ananitamani LIKE?
    8. Je ana ujasili wa kukabiliana na mazito mbeleni katika maisha?
    9. Je yupo tayari kunishika, kuniongoza, kunishauri, kunifundisha nisiyoyajua, atakuwa na muda na mimi na ataniombea?
    10. Je ataheshimu mawazo yangu na hisia zangu?
    11. Je ni mcha Mungu? Na anamuelekeo juu ya MUNGU?
    12. Je historia yake ikoje na ametoka wapi?
    13. Je kuna mipaka ipi katika upendo wetu?
    14. Je ameathika kweli juu yangu?

    KWA NINI TUNAPENDA NA TUNAPENDWA?
    Hakuna anayependa bila sababu na hakuna anayependwa bila sababu zinazomfanya.
    Mtu kupenda au kutopenda hata Mungu alikuwa na sababu za kuupenda ulimwengu hata
    Kumtoa mwana wa pekee ulumwenguni. Kupenda sio dhambi na kutopenda sio dhambi.
    Upendo ni ssehemu ya maisha na ni Mungu ambaye ameweka kwa mwanadamu Hivyo.
    Upendo umetoka kwa Mungu sio mtu ameamua kupenda jua kuwa upendo ni sehemu ya maishsa hata wanyama wanapenda na wana wivu wao kwa wao lakini upendo wa mwanadamu ni kubwa na unanguvu kuliko wanyama sababu nilizo nazo kwanini ninapenda na kwanini ninapendwa na ninani natakiwa kumpenda?
    (1) Kwa sababu naitaji kufarijiwa [nafsi]
    (2) Kwa sababu naitaji kukamilishwa [mwanz 2;18-]
    (3) Kwa sababu upendo ni nature
    (4) Kwa sababu ni mpango wa Mungu
    (5) Kwa sababu nahitaji kupendwa

    WATU WALIOSAHIHI WANAPATIKANAJE.
    Najua unaweza ukawa na swali kama hili, kutaka kujua nitawezaje kupata mume sahihi au mke sahihi katika maisha yangu?
    Jibu ni kwamba Mume au Mke aliye sahihi katika maisha yako “anatengenezwa na wewe mwenyewe na hili siyo kazi ya Mwanaume kama baadhi ya watu wanavyofundisha bali ni kazi ya watu wawili wanaopendana Mwanamke na Mwanaume. Mtu sahihi anaandaliwa mapema maana hata waswahili wanasema “Samaki mkunje angali mbichi” unajua hakuna timu nzuri kama haina wakufunzi wazuri. HIVYO:
    a) Mapenzi yanalelewa.
    b) Mapenzi yanatafutwa bila kuchoka.
    c) Mapenzi yanaandaliwa.
    d) Mapenzi yanapaliliwa (Kama shamba).
    e) Mapenzi yanatunzwa.
    f) Mapenzi ni shule kila siku.
    g) Mapenzi Yana mfano wa yai, yanashikwa kwa uangalifu wa hali ya juu sana, hayachuliwi na mtu mwenye akili za kitoto.
    h) Lazima ujue uthamani wake na umuhimu wake katika maisha ya mwanadamu.
    i) Mapenzi ni maisha yetu ya kila siku tuliyonayo.
    j) Mapenzi yanaishi ndani mtu aliyekubali kujifunza.
    k) Mapenzi ni matamu sana ukiyapatia
    l) Mapenzi ni machungu sana ukiyakosea.
    m) Mapenzi yanakaa kwa mtu anayetamani mabadiliko katika maisha yake.
    n) Mapenzi ni uzima katika moyo wa mtu akiyapatia.
    o) Mapenzi ni mauti na majuto ukiyakosea.
    p) Mapenzi yanaharibu heshima katika jamii ukiyakosea.
    q) Mapenzi yanaleta heshima katika jamii ukiyapatia
    r) Mapenzi ni kitabu kinachosomwa na kila mtu mdogo na mkubwa.
    s) Mapenzi ni bustani nzuri sana inayotengenezwa na mtu, analima, anapanda, anamwagilia maji na kuipalilia.
    t) Mapenzi ni maneno matamu yanayoweza kutekenya moyo wa mtu yasiyoweza kumboa mwenzi wako, yakumfanya afurahi, akijisikia kuheshimika, kutambulika, kukubalika, kuthaminika na kupendwa.
    u) Mapenzi hayana kiongozi bali katika mapenzi tunaongozana sisi kwa sisi..
    v) Katika mapenzi kila mtu anatakiwa kuwa kioo cha mwenzi wake, mrekebishe, mtengeneze, mfanye akubalike katika jamii iliyokuzunguka.
    w) Matengenezo ya mapenziyanahitaji muda (time) ya kutosha na mwenzi wako ukiwa na muda wa kutosha utaweza kumfahamu mwenzi wako akichukia anakuaje? Anapofurahi anakuaje? Hata kama kuna wengine huficha makucha yao unatakiwa kuto mitihani ili kufanya (teste) maana hakuna masomo yanayoweza kujifunza yakakosa mithani..
    x) Mtihani ni kipimo tosha cha kugundua uelewa wa mtu au mwenzi wako kuwa mtafika katika safari hiyo ya mapenzi au usitishe kutoendelea na safari.
    y) Mapenzi ni hadithi nzuri sana iliyokuwa na “mkato (,) nukta (.) na kiulizo (?)
    z) Mapenzi ni utiifu, unyenyekevu, upole, usikivu, na matendo.
    Mpendwa wangu ukiyajua hayo unaweza ukapata Mume au Mke mzuri sana katika maisha yako, mtengeneze mtu mwanzoni kabisa mwa mapenzi yenu kabla mapenzi hayajakomaa na kuota mizizi. Mimi Silvester Paulo niliyakosea mwanzoni niliumizwa sana, yakaharibu mfumo wangu wa maisha yangu. Hivyo nimewahi kuumizwa kimapenzi ijapokuwa ni Mtume, Mchungaji, mapenzi hayaangalii VYEO (TITLE) ulichonacho. (Mapenzi ni kitendawili kisichoweza kuteguliwa)” Huu ndio msemo wangu” Leo nimekuwa mwandishi wa vitabu na mwalimu baadaya kujifunza kivitendo. Mapenzi ni watu wawili tu na watatu ni Mungu msipoweza kusikilizana ninyi hakuna atakayeweza kukusaidia. Mtengeneze mwenzi wako kwa bidii sana kwa kuwa na muda naye wa kutosha, ukimfundisha, kumonya na kumuombea kwa Mungu ili aweze kuwa mtu wa kufaa kimaisha maana kuumizwa kimapenzi ni kuumizwa kimaisha
    UPO UWEZEKANO WA KUPATA MTU ASIYE SAHIHI KATIKA MAISHA YAKO
    Upo uwezekano mkubwa sana kuumizwa kimapenzi kutokana na tabia tofautitofauti na migongano isiyoweza kuepukika na inayoweza kuepukika.
    Mwanamke na Mwanaume sahihi kumpata sio mchezo ni historia maana mapenzi ya kweli ni “UTUMWA” mapenzi ya kweli yanatesa moyo wa mtu.
     
    JINSI YA UPATIKANAJI WA MTU ASIYE SAHIHI KATIKA MAISHA
    1. Hutumia hila wakisema kuwa Mungu amenionesha kuwa wewe ni mke au mume wangu hili ni moja ya njia wanapatikana madada wengi na wa kaka waliookoka.
    2. Wanatumia pesa zao wakijifanya wanakusaidia, wanakujali sana, wanakuthamini na kukuheshimu – kwamba wanakutafuta ili wayaumize maisha yako hawana mapenzi ya kweli.
    3. Wanatumia maumivu yako ya mapenzi Kama silaha ya kukupata.
    Mfano:
    Umewahi kutendewa mabaya na mwenzi wako uliyekuwa unampenda sana akakuumiza moyo huwa sasa wanajifanya kuwa ni
    a. Wafariji wa moyo wako.
    b. Waponyaji wa majeraha yako.
    c. Washauri wa karibu.
    d. Wanajionyesha kuwa wao wanajua mapenzi kuliko yule.
    Kumbe wanataka kutumia nafasi hiyo kukupata na wengi wamepatikana wanaumizwa zaidi.
    4. Wanatumia hali mbaya uliyonayo ya uchumi kifamilia kama njia ya kukupata wanatumia mambo yafuatayo:-
    a. Wanakutafutia mtaji- pesa, biashara nk.
    b. Wanaweza kuanza kulisha familia yako.
    c. Wazazi wako watatuzwa.
    d. Kununuliwa mavazi, chakula, afya yako, hata wanaweza kukujengea nyumba, kukununulia magari kumbe ni wauaji wa ndoto zako. madada wengi wamedanganyika na vijana wengi leo wanajutia.
    5. Wengine wanaingia kwa kishindo cha penzi la kweli kumbe lina unafiki ndani yake – muangalie Delila alivyomuingia Samsoni kumbe hakuwa na penzi la kweli alitafuta kujua siri ya nguvu za Samsoni na kumuangamiza wengi tumeumizwa hivyo kumbe mapenzi ni shule kubwa sana kila siku tunajifunza hakuna aliye mzoefu hata mmoja hasa swala hili la mapenzi Msemo nilionao kuhusu mapenzi Silvester Paul ni huu
     
    “TESO KUBWA SANA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU NI KUMPENDA MTU ASIYE SAHIHI KATIKA ENEO LILILOSAHIHI”
    YAPO MAMBO 25 YANAYOJITOKEZA:
     
    1. Mtu asiye sahihi huleta mahangaiko na mateso.
    2. Mtu asiye sahihi huleta majuto katika maisha.
    3. Mtu asiye sahihi huleta umasikini, taabu na maumivu.
    4. Mtu asiye sahihi huleta magonjwa ya moyo.
    5. Mtu asiye sahihi huleta roho ya kujichukia.
    6. Mtu asiye sahihi huvuta roho ya mauti ndani ya mtu.
    7. Mtu asiye sahihi huleta kilio kisichoisha ndani ya moyo wa mtu.
    8. Mtu asiye sahihi huleta kudharauliwa na matukano katika maisha yako.
    9. Mtu asiye sahihi huharibu heshima yako katika jamii.
    10. Mtu saiye sahihi huleta ogomvi usioisha katika familia.
    11. Mtu asiye sahihi hana toba ya kweli katika maisha yake.
    12. Mtu asiye sahihi anauwezo wa kukufanya uchukie kupenda na kupendwa katika maisha yako.
    13. Mtu asiye sahihi huleta ugumu wa maisha.
    14. Mtu asiye sahihi hupoteza maana yako ya kuishi na kusudi lako.
    15. Mtu asiye sahihi huondoa furaha na amani katika maisha yako.
    16. Mtu asiye sahihi anaharibu mtazamo wako wa kesho (future).
    17. Mtu asiye sahihi anakukosesha na watu walio sahihi maana ana roho za uongo, fitina, unafiki,wachoyo na rafiki wa maadui zako – mwangalie Delila akiwa na urafiki na wafilisti ambao walikuwa maadui za Samsoni Yuda Iskarioti anakuwa na urafiki na watu wenye uadui na Bwana Yesu.
    18. Mtu asiye sahihi anakutenga na Mungu wako.
    19. Mtu asiye sahihi anaweza kukufanya kupoteza uaminifu wako katika jamii na kufanya mambo yasiyostahili kama kutoka nje ya ndoa, kutoa talaka na kuwachukia watu jinsia Fulani kama wanaume au wanawake.
    20. Mtu asiye sahihi analeta maangaiko na mateso katika jamii
    21. Mtu asiye sahihi huleta sifa mbaya katika mazingira ya sifa njema.
    22. Mtu asiye sahihi huleta mipasuko na migongano katika familia.
    23. Mtu asiye sahihi hukwamisha ndoto za watu kutimia.
    24. Mtu asiye sahihi huharibu utaratibu wa maisha yako.
    25. Mtu asiye sahihi huvuta hofu, woga na mashaka katika eneo zima la kupenda na kupendwa katika maisha yako.
     
    HAZINA ZILIZOWEKWA CHINI YA ARDHI MIILI ILIYOZIKWA CHINI YA ARDHI ZILIZOWEZA KUTIMIZA NDOTO ZAO KWA SABABU YA KUWA NA WATU WASIO SAHIHI KATIKA ENEO LILILO SAHIHI
     
    Kuna watu wamekufa kwa sababu ya maumivu na mateso ya mapenzi, kusalitiwa, kutendewa vibaya na watu waliokuwa wanapenda kumbe walikuwa ni “Mbegu isiyosahihi katika eneo lililosahihi”.
    Wengine walikunywa sumu, wengine walijipiga risasi wakafa, wengine walijinyonga, wengine waliuawa maana walikuwa wanatafuta kitu sio penzi la kweli.Kuna miili mingi leo imezikwa hawajatimiza ndoto zao baada ya kupata watuwasio sahihi katika maisha yao. Wewe mwenyewe msomaji wangu unaushahidi mkubwa wa watu walio kufa kwa sababu ya mapenzi, katika Biblia unamuona Uria aliyekuwa mwanajeshi mkubwa tu katika serikaliya Mfalme Daudi siku moja Daudi alikuwa emepumzika juu ya gorofa yake kuangalia chini akamuona mke wa Uria anaoga akamtamani, akatuma wajakazi wake wakamlete ndani akamchukua na kulala naye alivyoona kuwa anamfaa akapanga mbinu jinsi Ulia afe ili aweze kumchukua yule mwanamke moja kwa moja akawaambia nendeni vitani na Uria mtangulizeni mbele ili afe, mbinu yake ikafanikiwa Uria akafa kabla ya ndoto yake kutimia unajuje kama angeweza kuwa mtu mkubwa sana baadaye mapenzi yanaweza kukwamisha ndoto za watu wengi sana.

JITAMBUE NA UISHI NA KUDUMU KATIKA MAHUSIANO YAKO KATIKA HICHI KITABU ..Men Are From Mars, Women Are From

By // No comments:

By // No comments:


  1. SOCIAL HALL
    SOCIAL HALL

    VYUO VIKUU BORA AFRICA




1 328 University of Cape Town South Africa 1039 568 352 267
2 462 Stellenbosch University South Africa 757 1120 214 454
3 474 Cairo University Egypt 760 449 1236 633
4 494 University of Pretoria South Africa 404 1247 162 608
5 563 University of the Witwatersrand South Africa 1383 1334 356 414
6 830 University of Kwazulu Natal South Africa 2013 1534 1349 559
7 855 University of Nairobi Kenya 330 2579 29 1400
8 1022 University of the Western Cape South Africa 1144 1827 990 1236
9 1050 American University in Cairo Egypt 1182 974 1149 2207
10 1074 University of South Africa South Africa 379 2131 465 1918
11 1167 Mansoura University Egypt 1423 1674 2878 1047
12 1178 University of Johannesburg South Africa 2544 3059 413 1004
13 1213 Makerere University Uganda 2177 3293 714 880
14 1341 Rhodes University South Africa 1622 1858 3122 1313
15 1401 Covenant University Ota Nigeria 3072 1154 925 2983
16 1419 Benha University Egypt 2194 1779 1415 2252
17 1448 Alexandria University Egypt 1142 3192 2961 996
18 1474 North West University South Africa 2274 4581 457 1229
19 1761 University of Ghana Ghana 3856 4204 1345 1451
20 1781 Université Djillali Liabes Algeria 8305 1336 4414 1850
21 1791 Obafemi Awolowo University Nigeria 963 2406 3825 2333
22 1798 Université Kasdi Merbah Ouargla Algeria 2229 2259 376 3826
23 1803 Addis Ababa University Ethiopia 1954 5885 837 1444
24 1822 University of Namibia Namibia 2009 2666 1815 2630
25 1868 Nelson Mandela Metropolitan University South Africa 4181 2696 3272 1759
26 1874 Kwame Nkrumah University of Science & Technology Ghana 3195 4754 693 1944
27 1918 University of Khartoum Sudan 47 5967 2214 2094
28 1922 Zagazig University Egypt 2698 5333 1645 1374
29 2026 Assiut University Egypt 2867 6368 1443 1280
30 2044 University of the Free State South Africa 3094 4746 3009 1339
31 2292 Kafrelsheikh University Egypt 1013 5609 3751 1798
32 2295 University of Zambia Zambia 3330 7563 824 1749
33 2297 Université Abou Bekr Belkaid Tlemcen Algeria 2049 6955 488 2477
34 2310 University of Ibadan Nigeria 5659 4795 3294 1487
35 2321 Université Constantine 1 (Ex Université Mentouri) Algeria 2188 7018 1041 2094
36 2384 Cape Peninsula University of Technology South Africa 4207 5322 1502 2333
37 2475 University of Dar Es Salaam Tanzania 3215 4368 4473 2094
38 2491 Kenyatta University Kenya 891 6422 2515 2477
39 2507 Université Cheikh Anta Diop de Dakar Senegal 6393 4820 3471 1822
40 2542 University of Zimbabwe Zimbabwe 5120 6125 2401 1839
41 2554 Université des Sciences et de la Technologie Houari Boumediene Algeria 4907 6571 2736 1589
42 2565 Minia University Egypt 2244 8709 1824 1711
43 2597 University of Lagos Nigeria 6137 4448 3273 2252
44 2624 Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology Kenya 2105 7283 1335 2564
45 2742 University of Ilorin Nigeria 3802 7486 986 2586
46 2795 University of Botswana Botswana 4384 6035 2989 2252
47 2827 Université Mohammed V Souissi Morocco 2938 8197 1163 2586
48 2886 Suez Canal University Egypt 3291 9776 3172 1243
49 2957 Durban University of Technology South Africa 640 6695 1966 3695
50 2973 Helwan University Egypt 2481 6740 5234 1973
51 2984 Ain Shams University Egypt 1409 11953 4139 851
52 3052 University of Tanta Egypt 3595 7825 5316 1526
53 3125 Universidade Eduardo Mondlane Mozambique 6499 4791 4897 2564
54 3142 Université Mohamed Khider Biskra Algeria 2978 8920 659 3272
55 3150 University of Mauritius Mauritius 5196 6509 3384 2494
56 3176 Sudan University of Science & Technology Sudan 3900 7904 557 3596
57 3206 Misurata University (Misrata University) Libya 1857 749 12377 5414
58 3219 Université Mohammed V Agdal Morocco 6472 8497 4693 1389
59 3289 Minufiya University Egypt 2294 8821 6364 1580
60 3303 Egerton University Kenya 4235 6243 2698 3272
61 3328 Université Cadi Ayyad Marrakech Morocco 5889 11165 2871 1248
62 3378 Arab Academy for Science & Technology and Maritime Transport Egypt 1223 5908 6685 2983
63 3416 Fayoum University Egypt 3534 10215 3359 1904
64 3424 University of Agriculture Abeokuta Nigeria 5486 9213 1062 2983
65 3573 Moi University Kenya 6322 9124 2620 2438
66 3597 (1) University of Zululand South Africa 3285 8711 2354 3200
67 3599 Ahmadu Bello University Nigeria 5788 9029 3002 2459
68 3621 Université Hassiba Ben Bouali Algeria 1962 10481 2371 2793
69 3701 Polytechnic of Namibia Namibia 1856 6113 2979 4421
70 3715 Université de Batna Algeria 5747 8734 3195 2630
71 3784 Jimma University Ethiopia 9792 7654 3683 2377
72 3785 Université Mouloud Mammeri de Tizi Ouzou Algeria 6673 10086 2262 2477
73 3872 Federal University of Technology Akure Nigeria 5111 10508 1679 2891
74 3877 Strathmore University Nairobi Kenya 64 5227 5761 5414
75 3887 University of Cape Coast Ghana 5026 8609 1405 3826
76 3966 South Valley University Egypt 4797 9284 6169 2041
77 4001 University of Fort Hare South Africa 8327 7856 5961 2162
78 4022 Landmark University Nigeria 6611 2293 6119 5414
79 4059 Université Setif 1 Ferhat Abbas Setif Algeria 5984 10586 3453 2309
80 4064 Tshwane University of Technology South Africa 7966 5932 11175 1867
81 4094 (1) Université Mohammed Premier Oujda Morocco 6674 9932 7966 1322
82 4100 University of Nigeria Nigeria 8506 6774 6503 2513
83 4199 German University in Cairo Egypt 8883 7958 5010 2564
84 4230 Université d’Alger 1 Algeria 6255 8379 1544 4158
85 4233 University of Limpopo South Africa 12784 8444 3740 2333
86 4244 Sokoine University of Agriculture Tanzania 8905 9263 5063 2137
87 4269 Université Hassan II Ain Chock Morocco 1317 9770 13206 1557
88 4402 Mbarara University of Science & Technology Uganda 12742 5409 10269 2041
89 4412 Université Virtuelle de Tunis Tunisia 3929 5624 2664 5414
90 4462 University of Benin Nigeria 7132 7488 5581 3133
91 4463 Université d’Oran Algeria 11004 9683 3054 2564
92 4491 Université de Bejaia Algeria 6262 10476 5159 2309
93 4590 University of Port Harcourt Nigeria 10326 6649 5462 3133
94 4630 Université des Sciences et de la Technologie d’Oran Mohamed Boudiaf Algeria 7806 10687 4880 2252
95 4642 (1) Muhimbili University of Health and Allied Sciences Tanzania 7238 14459 2521 1684
96 4644 Federal University of Technology Minna Nigeria 7218 11522 805 3695
97 4661 Université Abdelhamid Ibn Badis Mostaganem Algeria 3743 9252 7095 2793
98 4691 University Shendi Sudan 10333 2004 8233 5414
99 4704 National University of Science & Technology Zimbabwe 5106 11432 2964 3039
100 4786 Al Akhawayn University Ifrane Morocco 4564 5737

FAHAMU HOMA YA MANJANO NA JINSI YA KUJIKINGA

By // No comments:
HOMA YA MANJANO
 
SOCIAL HALL
SOCIAL HALL
CHANZO, ATHARI  , KINGA   NA  TIBA  YA  UGONJWA  WA  MANJANO.
Ugonjwa    wa  Manjano    ambao  hufahamika  kitaalamu  kama  HEPATITIS  B  ni  hatari  sana  na  umesababisha  vifo  vya  mamilioni  ya  watu  duniani  kote.    Kwa  mujibu  wa  ripoti  ya  Shirika  la  Afya  Duniani  ( W.H.O )   kuna  zaidi  ya  wau  Milioni  350  duniani  ambao  wameathiriwa  na  ugonjwa  huu  hatari   kabisa  na  zaidi  ya  watu  620,000  hufa  kila  mwaka  kwa  ugonjwa  wa  Manjano.

CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO

Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (  HBV )  ambavyo  hushambulia    zaidi ini  la  mwanadamu.   Virusi  hivi  visipo  tibiwa  mapema  hutengeneza  uvimbe  katika  ini  na  kusababisha  asratani  ya  ini  ambayo  hupelekea  kifo.
MAMBO  YASABABISHAYO  MAAMBUKIZI  YA  UGONJWA  WA  MANJANO.

Ugonjwa    wa  Manjano  huambukizwa  kwa  njia  zifuatazo  :
i.                   Kujamiiana  bila  kutumia  kinga.
ii.                Kunyonyana  ndimi
iii.             Kuchangia  damu  isiyo  salama
iv.             Mama  mjamzito mwenye  ugonjwa  huu  anaweza  kumuambukiza  mtoto  wake  wakati  wa  kujifungua.
v.                Kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  vile  wembe  na  sindano.

                        DALILI  ZA  UGONJWA  WA  MANJANO
Dalili  za  ugonjwa wa  manjano  huchukua  muda  mrefu  kuonekana  tangu  maambukizi  yatokee, na  zinapo  anza  kuonekana  wazi  wazi, mgonjwa  anakuwa  amesha  athirika  kwa  kiwango  kikubwa  sana.  Dalili  za  ugonjwa   huu  ni  kama  ifuatavyo :
i.                     Uchovu  wa  mwili
ii.                Kichefuchefu
iii.             Mwili  kuwa  dhaifu
iv.             Homa  kali
v.                 Kupoteza  hamu  ya  kula
vi.             Kupungua  uzito
vii.          Kupatwa  na  maumivu  makali  ya  tumbo upande  wa  ini.
viii.       Kukojoa  mkojo  wa  rangi  nyeusi
ix.              Macho  na  ngozi  kuwa  vya  njano.
                        KINGA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
i.                    Kupatiwa  chanjo  ya  kujikinga  na  maambukizi  ya  ugonjwa  huu.
ii.                Kutumia  kinga  wakati  wa  kujamiiana
iii.             Kuacha   kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  sindano, wembe  n.k
iv.             Kutochangia  mswaki
v.                Kuwa  na  mpenzi  mmoja  mwaminifu
vi.             Kuto ongezewa damu  ambayo  haijapimwa  na  kuthibitika  kuwa  salama.

                     TIBA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi  hospitali  atapatiwa  dawa za  kupambana  na  virusi  kuvipunguza  nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini  lililoathirika  huondolewa  na  kuwekwa  jingine  japo  ni  vigumu  kupata  ini  salama.
Ukisha  gundua  kuwa  umeambukizwa  ugonjwa  huu  unashauriwa   kuacha  kutumia  pombe, dawa  za  kulevya  na  vitu  vingine  vinavyo  athiri  utendaji  kazi  wa  ini.
Mr.Kikoti. Powered by Blogger.

Comments