UGONJWA HATARII WA KIFAFA CHA MIMBA

By // No comments:
KIFAFA CHA MIMBA
SOCIAL HALL
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions).

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo
yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.
Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada
ya kujifungua.

SABABU ZINAZO PELEKEA TATIZO HILO.

Sababu la tatizo bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua. Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili
(Predisposi ng factors). Baadhi ni pamoja na



1.Mwanamke kuwa na wenza wengi hali inayopelekea muingiliano wa Chromosomes.

2.Sehemu moja ya ubongo kuwa na damu nyingi kuliko nyingine na kupelekea shinikizo la damu kuwa kubwa katika ubongo.
3 Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35. 
4 Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.
 
5 Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.
 
6 Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.


SABABU NYINGINE PIA NI KAMA

 1.wanawake wote wenye mimba za kwanza
2.mimba za mapema kabla ya 20
3. wanawake ambao wazaz,bib au ndg zao wa karbu waliwah kupatwa na matatzo ya kifafa katka mimba zao
4. wanawake walev hasa wakiwa wajawazito
5.wavutaj wa sigara
6. wanawake wenye visukar
7.wanawake wenye presha
8.mimba za uzeeni baada ya miaka 35
9.wanawake wenye tabia ya kubadlisha badlisha wanaume
10.wanawake waliopatwa na kfafa mimba zao za kwanza kuna hatar kukpata kifafa tena mimba znazofuata
11.mimba za mapacha
12.kuzaa mara nyingi

DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA

1.Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).


2.Shinikizo la damu kupanda.


3.Kuwa na protein katika mkojo.


4.Kizunguzungu na macho kuoana giza.


5.Kifafa chenyewe cha mimba.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.


1.Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.


2.Kuzaa mtoto mfu.


3.Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)


4.Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)


5.Kuzaa mtoto mwenye uzito
pungufu.


SULUHISHO

 1.Kujifungulia katika kituo cha afya.


2.Kuhudhuria Klinik wakati wa ujauzito.


3.Kumuona daktari unapokuwa na viashiria vya hatari wakati wa ujauzito kama kuvimba miguu au shinikizo la damu kupanda

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI NA MWANAMKE WAKATI WA HEDHI.

By // No comments:
SOCIAL HALL
SOCIAL HALL

Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana..Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi...Zifuatazo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake{period}.. 

 MADHARA KWA MWANAUME.
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

 2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

 3.Kuziba kwa njia ya mkojo.

 4.Utasa au ugumba.

 5.Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

 6.Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.


MADHARA KWA MWANAMKE.
1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

 2.Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

 3.Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

 4.Utasa au Ugumba.

 5.Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

 6.Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka KU-DO.
NOTE
 Hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

DOWNLOAD AND LISTEN KABOY-BUSH BOY.MP3....Philemoni Sadiki

By // No comments:

SOCIAL HALL

DOWNLOAD NA SIKILIZA HAPA
http://www.audiomack.com/artist/emma-kikoti

WANAMAHESABU BORA ZAIDI DUNIANI WALIOWEKA HISTORIA KATIKA SEKTA YA HESABU

By // No comments:

MAMBO HAYA NDIYO YANAWAFANYA WATU WAACHE KUFATILIA MAPENZI YENU

By // No comments:

MAHUSIANO
SOCIAL HALL
Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.  Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.

1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:  Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.

2. Upekee wa mambo:  Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.

3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua. 

4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza  kuzitumia kupata suluhu ya tatizo. 

5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa  nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine. 

6. Kuweni peke yenu:
Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni  kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi.  Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao  kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.

7. Nenda ‘darasani’ :  Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu. Mfano wa makala unazoweza kusoma ni kama vile

DALILI ZA MSICHANA MWENYE MIMBA{UJAUZITO}

By // No comments:
KUJUA KAMA MSICHANA NI MJAMZITO
SOCIAL HALL MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

“Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

Zifuatazo ni dalili ambazo baba au kijana ukiziona kwa mkeo basi usifikilie tofauti wala kuanza kuishi nae tofauti na awali kwani si yeye ni kiumbe chake alichobeba kwenye mwili wake...


Maumivu kwenye matiti.
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini
Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kutokwa damu bila kutegemea
"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Ambaye anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito..

Kuchoka
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi” anasema Goist.

Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Mwili kuvimba

Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
 
Tamaa ya vitu mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Kuwa na hasira
"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist

Kuongezeka kwa joto mwilini
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
ANGALIZO:
Si kila msichana anaweza akafanya mambo haya la hasha ni baadhi yao huwa wanafanya hivi na mara nyingi ni kwa wale wenye mimba za mwanzo..

UCHUMI NI NINI...?? {SOMO LA UCHUMI}

By // No comments:



Uchumi ni jumla ya shughuli zote za kibinadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji ya watu. Ni hasa shughuli za uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.

Uchumi mara nyingi hutazamiwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia.

Uchumi Mkuu: (macroeconomics) ni elimu juu ya picha kamili ya uchumi, yaani njia ambayo utajiri unapatikana na unagawanywa. Inaweza kuwa elimu kuhusu nchi maalum au dunia nzima na jinsi tofauti zinavyoingizwa katika picha nzima ya dunia. Kuna majadiliano kama ya:

bullet
Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kuwa masikini zaidi. Tufanye nini kuhusu jambo hili?
bullet
Serikali ijiingize kiasi gani katika uendeshaji wa soko huru?
bullet
Kwa kuzingatia na uharibifu wa mazingira, je, ukuaji wa uchumi usiodhibitiwa unatakiwa?


SOCIAL HALL
Uchumi Mkuu Imara (Macroeconomic Stability) ni matokeo ya kuwa na kodi ya hazina, sera za fedha na kiwango cha kubadilishana fedha inayokusudia kufikia malengo ya uchumi mkuu kama vile ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, madeni ya nje na akiba halisi ya kimataifa.
Uchumi Mdogo (Microeconomics) ni elimu kuhusu jinsi viwanda, sekta fulani, biashara au kaya zinavyofanya kazi.
Jumla ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product - GDP) ni kipimo cha jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana nchini katika muda maalum. Kwa maneno mengine Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa fedha. Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1% zaidi kuliko ya mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1%. Lakini jumla ya pato la taifa (GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa – kwa mfano, uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi yao.
Jumla ya Pato la Taifa (GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.
Ukuaji Halisi (Real Growth): Kwa vipengele vyote viwili jumla ya pato la utajiri (GDP) na ukuaji wa pato la utajiri (GNP), kama ukuaji ni asilimia 7% kwa mwaka, lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5% basi Ukuaji Halisi ungekuwa asilimia 2% tu kwa mwaka.
Mfumuko wa Bei (Inflation): Kipimo cha kupanda kwa bei kati ya mwaka mmoja na mwaka unaofuata – hasa ukizingatia wazo la kupata vifaa vya madukani/sokoni.
Mtaji wa jamii (Social Capital) ni kama “gundi” inayounganisha pamoja familia, makundi na jumuiya. Inahusisha imani, desturi na tabia za jamii ambazo husaidia kufanya kazi pamoja kwa uthabiti katika makundi yaliyo rasmi na yasiyo rasmi.
Vyama vya Jumuiya (Civil Society Organisation):Inahusisha vyama rasmi ambavyo vimesajiliwa na serikali na vile visivyo rasmi. Vyama hivyo ni pamoja na vile vya hisani, dini, vya shughuli maalumu, kundi shawishi, kitaaluma, na vyama vya makundi maalumu kama vile vyama vya wafanyakazi na vyama vya wanafunzi. Vyama visivyo rasmi ni pamoja na Upatu, vyama vya makabila, mpira wa miguu ambavyo vinaundwa na vijana wa kiume na netiboli vinavyoundwa na vijana wa kike.
Matayarisho Ya Bajeti inayozingatia maskini (Pro-poor Budgeting): na usimamizi wa matumizi (and expenditure monitoring). Fedha zinatengwa katika bajeti kwa ajili ya programu zinazowalenga watu masikini. Lakini fedha hizi zinapaswa kupitia Hazina, wizara inayohusika, serikali za Mikoa na Halmashauri za Wilaya/ Miji na kitengo cha huduma (k.m. shule au hospitali) kabla ya mtu masikini kupata faida. Kwa usimamizi thabiti fedha hizi zinaweza kutumika vizuri.
Mapitio ya Matumizi ya Serikali (Public Expenditure Review). Timu ya Matumizi ya Serikali hukutana mara moja kila baada ya majuma mawili ili kutafakari jinsi serikali inavyopata na kutumia fedha zilizo kwenye bajeti. Timu hii iliundwa mwaka 1997 inawajumuisha viongozi wakuu wa serikali na wawakilishi kutoka katika jumuiya ya wafanyabiashara, makundi ya jumuiya na makundi ya wafadhili wa nje.

Bajeti za Serikali (Government Budgets). Serikali ni kama familia ambayo inapaswa kuweka uwiano kati ya fedha zinazoingia na fedha zitumikazo. Kama hakuna fedha zinazoingia serikali inapaswa kuamua itumie kiasi gani na isitumie kiasi gani. Utaratibu wa kukusanya taarifa hii na kufanya uamuzi ndiyo huitwa Bajeti
Njia za Mapato ya Serikali (Source of government income):

bulletKodi ya moja kwa moja k.m. kodi ya mapato, kodi ya mali
bulletKodi isiyo ya moja kwa moja k.m. kodi ya ushuru wa forodha, kodi ya mauzo
bulletMapato yasiyo na kodi k.m. liseni na ada
bulletMikopo k.m. toka Mashirika ya Fedha Duniani na Benki ya Dunia ·
bulletMisaada k.m. toka serikali nyinginezo na toka mashirika yasiyo ya kiserikali
Kuongeza kodi ni jambo lisilopendwa na baadhi ya kodi nyingine ni mzigo mkubwa kwa watu masikini kuliko watu matajiri. Mikopo ni mizuri kuziba mapengo ya muda mfupi na kuanzisha biashara mpya, lakini lazima mikopo hiyo ilipwe. Misaada inakaribishwa bali hatuwezi kupata misaada wakati wote.
panya-21.jpg (18491 bytes)
Mishahara na Gharama Nyinginezo (Personal Emoluments (PE) and other charges (OC)): Wizara inatumia sehemu ya bajeti yake kwa mishahara na sehemu nyingine kulipia gharama nyinginezo. Kama sehemu ya kutekeleza waraka wa Upunguzaji wa Umasikini (PRSP), Serikali itaongeza bajeti ambayo inatengwa kwa ajili ya gharama za matumizi mengine – kwa mfano, kati ya mwaka 1999/2000 hadi 2002/2003 bajeti itaongezwa toka asilimia 2 hadi 3.8% kwa ajili ya elimu ya msingi na toka asilimia 2.1 hadi 3.8% kwa ajili ya Afya ya Jamii.




VIFUPISHO VYA KIUCHUMI
BoT Bank of Tanzania – Benki Kuu (ya Tanzania)


CAS Country Assistance Strategy – Mbinu za Kusaidia Nchi
CSO Civil Society Organisation – Jumuiya Hiari za Wananchi
DED District Executive Director – Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
ELCT Evangelical Lutheran Church of Tanzania – Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
ESAF Enhanced Structural Adjustment Facility – Uharakishaji Mabadiliko ya Kimuundo
GDP Gross Domestic Product – Pato Ghafi la Ndani
GNP Gross Nationa Product – Jumla ya Pato la Taifa
HBS Household Budget Survey (1991/92) – Mapitio ya Bajeti za Kaya (1991/92)
HIPC Highly Indebted Poor Countries – Nchi Masikini zenye Madeni Makubwa
HRDS Human Resource Development Survey (1993) – Ukaguzi wa Maendeleo ya Nguvu kazi (1993)
HRS Human Resource Survey (1983) – Ukaguzi wa Nguvu kazi
IBRD International Bank for Reconstruction and Development (World Bank) – Benki ya Dunia ya Urekebishaji na Maendeleo
IFMS Integrated Financial Management Information System – Mfumo wa Pamoja wa Taarifa za Uendeshaji wa Fedha
IMCI Integrated Management of Childhood Illness – Uendeshaji wa Pamoja wa Magonjwa ya Watoto
IMF International Monetary Fund – Shirika la Mfuko wa Fedha Duniani
LGRP Local Government Reform Programme – Mpango wa Mageuzi wa Serikali za Mitaa
M & E Monitoring and Evaluation – Usimamizi na Tathmini
MDF Multilateral Development Fund – Mfuko wa Shughuli mbali mbali za Maendeleo
MSME Micro, Small and Medium Enterprises – Viwanda Vidogo na vya Kati
MTEF Medium-term Expenditure Framework - Muundo wa Matumizi ya Muda wa Kati

NBS National Bureau Statistics – Kitengo cha Taifa cha Takwimu
NGO Non-Government Organisation – Shirika lisilo la Kiserikali
NPES National Poverty Eradication Strategy – Mpango wa Taifa wa Mkakati waKupunguza Umasikini
OPM Oxford Policy Management – Manejimenti ya Oxford kuhusuSera ya Uongozi
PER Public Expenditure Review – Mapitio ya Matumizi ya Serikali
PL Poverty Line – Mstari wa Umasikini
PMI Poverty and Welfare Monitoring Indicators – Viashirio vya Uratibishaji wa Umasikini na Usawa
PPA Participatory Povery Assessment (1995) – Tathmini ya Ushirikishwaji juu ya Umasikini
PRGF Poverty Reduction and Growth Facility – Mfumo wa Ukuaji na Upunguaji wa Umasikini
PRSC Poverty Reduction Support Credit – Mikopo ya Kusaidia Kupunguza Umasikini
PRSP Poverty Reduction Strategy Paper – Mkakati wa Mbinu za Upunguzaji Umasikini
PSAC-I Programme Structural Adjustment Credit – Programu ya Mikopo ya Urekebishaji Miundo
PSRP Public Service Reform Programme – Programu za Mageuzi ya Huduma za Umma
RAS Reginal Administrative Secretaries – Makatibu Tawala wa Mikoa
SME Small to Medium Enterprises – Viwanda Vidogo hadi vya Kati
TAS Tanzania Assistance Strategy – Mbinu za Kusaidia Tanzania
TIC Tanzania Investment Centre – Kituo cha Uwekezaji Tanzania
TIPER Tanzania-Italian Petroleum Refinery – Mtambo wa Kusafisha Mafuta Tanzania na Italia
TRCHS Tanzania Reproductive and Child Health Survey (1999) - Mpango wa Uzazi na Afya ya Watoto
TSED Tanzania Socio-Economic Database – Mfumo wa Utunzaji wa Taarifa za Jamii na Uchumi
TTC Teacher Training College – Chuo cha Ualimu
VPO Vice President's Office – Ofisi ya Makamu wa Rais

UMUHIMU WA MAJI KWA AFYA NA DAWA

By // No comments:
UMUHIMU WA MAJI

SOCIAL HALL

Mwili wa binadamu unajumuisha asilimia 25 za vimumunyishwaji (solute) na asilimia nyingine 75 ni vimumunyishaji (solvent). Tishu za ubongo zinasemwa kuwa na mpaka asilimia 85 za maji. Wakati awamu za kudadisi mwili wa binadamu zilipoanza, sababu ya vigezo vya kisayansi na kwa uelewa mkubwa katika kemia ulipofikiwa, moja kwa moja ilikuja kudhaniwa kwamba uelewa ule ule ambao ulifikiwa katika kanuni za kikemia ukahusishwa na vimumunyishwaji vya mwili.

Kwahiyo ilichukuliwa kuwa vimumunyishwaji (mifupa na nyama nyama za mwili) ndivyo vinavyodhibiti kazi zote za mwili. Mwanzoni kabisa mwa tafiti juu ya mwili wa binadamu, maji ya mwili yalichukuliwa tu kama kimumunyishaji, kiziba nafasi na kama njia tu ya kusafirishia – mawazo sawa na yaliyozalishwa katika majaribio ya kitesti tyubu. Hakuna kazi zingine mhimu za maji zilizojadiliwa kuhusiana na maji (the solvent). Uelewa wa msingi katika utabibu katika nyakati hizi – ambao umerithiwa toka programu za kielimu zilizoanzishwa mwanzoni katika kisomo cha mfumo (systematic learning) pia huvichukulia vimumunyishwaji (nyama na mifupa) kama ndivyo vinavyodhibiti mwili na vimumunyishaji (maji ambayo ndiyo asilimia 75 ya mwili) kama njia tu ya kusafirishia malighafi mwilini. Mwili wa binadamu sasa unafikiriwa kuwa ni testityubu kubwa iliyojazwa vitu vigumu (nyama na mifupa) vya asili tofauti tofauti.

Katika sayansi, imedhaniwa kuwa ni vimumunyishwaji (vitu ambavyo huyeyuka au kubebwa katika damu na umajimaji ndani ya mwili) ndivyo ambavyo huzidhibiti na kuziongoza kazi zote zinazofanywa na mwili. Hii inajumuisha pia udhibiti wa kiasi cha maji cha mwili (the solvent) ambacho mpaka sasa imefikiriwa kuwa kinadhibitiwa vizuri na mwili. Imedhaniwa hivyo sababu maji yanapatikana kirahisi tu na hayauzwi kivile, hivyo mwili hauwezi kupungukiwa na kitu ambacho kinapatikana kirahisi!.

Chini ya dhana hii potofu, tafiti zote kuhusu mwili wa mwanadamu zimeelekezwa katika kutafiti kitu chochote fulani ambacho kinadhaniwa ndicho kinachosababisha ugonjwa fulani. Kwahiyo, vyote vinavyodhaniwa kuwa na uwezekano wa kusababisha ugonjwa fulani na mabadiliko ya kielementi vimejaribiwa bila suluhisho lenye jibu moja hata katika ugonjwa fulani mmoja. Kwa hali ilivyo, matibabu yote ni kwa ajili ya kutuliza au kupunguza maumivu tu na siyo yenye uwezo wa kuponya au kutokomeza tatizo (isipokuwa kwa maambukizi ya bakteria na kwa matumizi ya viua vijasumu/antibiotics). Shinikizo la juu la damu/BP bado halitibiki, wagonjwa wa BP huishi wakitibiwa mpaka watakapokufa, matibabu na uangalifu juu ya BP vinaendelea kuwa sehemu ya maisha ya mtu. Pumu/asthma haitibiki, dawa vipumuzi (inhalers) ni marafiki wa waathirika wa asthma. Vidonda vya tumbo havitibiki dawa za kudhibiti asidi (antiacids) ni lazima ziwe karibu na mgonjwa. Mizio/aleji haitibiki, waathirika muda wote wanaishi kwa dawa. Maumivu ya mishipa hayatibiki na hatimaye inaweza kumfanya mtu kiwete na kadharika.

Kwa kuegemea dhana hii ya mwanzo juu ya kazi za maji mwilini, imekuja kuzoeleka kuchukulia kitendo cha mdomo uliokauka kuwa ndiyo ishara za mwili kuhitaji maji au kuwa na kiu cha maji ambayo imedhaniwa zaidi kuwa yanadhibitiwa vizuri ikiwa hisia za kukauka mdomo hazitokei – kwa sababu pengine maji ni bure na yanapatikana kirahisi. Hili ni kosa la kipuuzi na ni dhana inayoleta mkanganyiko mkubwa katika taaluma ya kitabibu na ndiyo inayohusika katika suala zima la kukosa mafanikio katika kupata suluhisho la kudumu katika kuzuia na kuponya magonjwa katika mwili pamoja na tafiti zote hizo na zenye gharama kubwa.

Dr. Batmanhelidj tayari amechapisha chapisho lake juu ya utafiti wa ki-kliniki wakati alipotibu zaidi ya watu 3000 waathirika wa vidonda vya tumbo kwa kutumia maji pekee. Anasema aligunduwa kwa mara ya kwanza katika taaluma ya kitabibu kuwa ugonjwa huu maarufu wa vidonda vya tumbo ukiitika wenyewe kwa maji pekee. Ki-kliniki inajitokeza hali hiyo kufanana na ‘ugonjwa kiu’. Chini ya mazingira hayo hayo na katika mazingira ya ki-kliniki, dalili zingine za magonjwa zilionekana zikiitika zenyewe kwa maji pekee. Utafiti mkubwa umethibitisha uchunguzi wa ki-kliniki wa dr.Batman kwamba mwili una miliki ishara changamano kabisa za ishara za kiu – mfumo ishara shirikiano wakati wa udhibiti wa kiasi cha maji kinachopatikana wakati wa upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kwa mjibu wa maelezo ya dr.B, kanuni zinazodhibiti tafiti kuhusu afya ya mwili wa binadamu ni lazima zibadilishwe ikiwa tunataka kuyashinda magonjwa. Ukweli unajionesha wazi sasa kuwa taaluma ya madawa inaegemea katika dhana za uongo na vigezo visivyo kamili. La! sivyo, inawezekanaje mfumo mchafuko wa ishara kwa ajili ya umetaboli wa maji ukosekane? au udharauriwe kidhahiri kwa muda mrefu hivi? kwa muda uliopo; ‘mdomo uliokauka’ ndiyo ishara pekee inayokubalika kama ishara ya upungufu wa maji ya mwili. Kama ilivyofafanuliwa, ishara hii ya mdomo ukauke ni ishara ya mwisho kabisa ya mwili kuhitaji maji. Madhara makubwa kiafya yanajitokeza mwilini kabla ya ishara ya mdomo kukauka. Watafiti wa mwanzo watakuwa walitambuwa kuwa ili kuwezesha tendo la kutafuna na kumeza, mate huzarishwa hata kama sehemu zingine za mwili zimepungukiwa na kiasi kikubwa cha maji.

Upungufu sugu wa maji mwilini (chronic dehydration) ndio chanzo cha magonjwa mengi kwa mwili wa binadamu ambayo kisababishi chake kilikuwa hakijulikani mpaka sasa. Rejea katika kitabu chochote cha kitabibu utaona kurasa nyingi zenye maelezo mzunguko, lakini linapokuja suala la kutoa sababu katika magonjwa makuu ya mwili, jibu kwa hali zote ni sare na fupi kabisa: ‘sababu za chanzo chake hazijulikani’ (etiology unknown).

Kwa asili, upungufu sugu wa maji mwilini unamaanisha upungufu wa kudumu wa maji ambao umedumu kwa muda fulani. Kama ilivyo kwa maradhi ya upungufu wa kiini lishe fulani, mfano upungufu wa vitamini C kwa ugonjwa wa kiseyeye (scurvy), upungufu wa vitamini B kwa ugonjwa wa beriberi au upungufu wa madini ya chuma kwa ugonjwa wa anemia, upungufu wa vitamini D kwa ugonjwa wa matege/nyongea na mengine unayoyafahamu; namna mahususi ya kutibu magonjwa hayo ni kurudishia kilichopunguwa. Kwa mjibu huu, ikiwa tutaanza kutambua mkanganyiko wa kiafya uletwao na upungufu wa maji, uzuiwaji wake na hata uponyekaji wake wa mwanzo utakuwa ni rahisi.

Wakati mwili wa binadamu ulipokua toka katika spishi (species) ambazo zilipewa maisha katika maji, utegemezi sawa wa sifa ya maji katika uzima ulirithiwa. Umhimu wa maji katika miili ya spishi hai akiwemo binadamu haujabadilika tangu uumbwaji wa kwanza wa maisha katika maji chumvi na hatimaye katika kuzoea kwake katika maji baridi.

Wakati maisha yalipoanza kufanyika katika ardhi, kuliundwa mfumo maalumu ili kudhibiti kiasi maalumu cha maji mwilini kwa ajili ya makuzi zaidi ya spishi. Prosesi hii ya mabadiliko ya muda ya kuzoea mazingira ya kubana matumizi ya maji ilirithiwa na kuwa kama mfumo uliojijenga vizuri katika mwili wa binadamu na ndio sasa ni muundombinu mhimu katika mifumo ya ufanyaji kazi ndani ya mwili wa binadamu wa nyakati hizi.

Menejimenti ya kiasi kidogo cha maji kinachopatikana mwilini ikatokea kuwa ni jukumu la mfumo mkanganyiko (complex system). Usawa huu wa mfumo mkanganyiko wa mgawo na usambazaji wa maji hubaki katika kazi hiyo mpaka mwili utakapopata ishara kamili zisizo na shaka yeyote za kupatikana kwa maji ya kutosha. Kwakuwa kila kazi ya mwili hudhibitiwa na kutupwa katika mtiriiriko wa maji, ‘menejimenti ya maji’ ndiyo namna pekee ya kuhakikisha kwamba kiasi cha kutosha cha maji na viini lishe vinavyosafirishwa nayo, kinayafikia kwanza ogani mhimu ambazo zinatakiwa kukabiliana na mfadhaiko wowote mpya. Mfumo huu umejitokeza zaidi na zaidi kwa ajili ya kuendelea kuishi dhidi ya maadui wa asili na wawindaji wengine wa afya ya binadamu. Ni mfumo mhimu kabisa katika mazingira ya kutaka kupaa ama kupigana: bado ni mfumo unaoendelea hata katika maisha yetu ya uchumi wa soko huria.

Tunaweza kufupisha hapa kuwa, kutokana na mazoea yetu ya kusubiri kiu au mdomo ukauke ndipo tunywe maji, huwa tunaulazimisha mwili kuishi katika mfumo wa mgawo wa maji na hatimaye usambazwaji wake, mfumo huo ndio huleta balaa mwilini kwa kuzarisha ishara mbalimabali za magonjwa ambayo dawa yake pekee ni kubadilika kwetu na kuanza kunywa maji kabla ya kusikia kiu na kujifunza umhimu wa maji kwa maisha marefu bila magonjwa.

SOCIAL HALL


MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA TIBA YA MAJI: Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1=miligramu 31.25
Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.


Pengine umeshageuza kichwa na kunisema, “Wewe ni kichaa.....hicho ni kiasi kingi sana cha maji”. Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, glasi 8 za maji zikigawanywa mara nane kwa siku (glasi 1 = ml ujazo wa maji utakaotakiwa kunywa kwa wakati mmoja).

Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:

·
Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75x2.2=aunsi 165.· Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2=aunsi 82.5.· Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8=aunsi 10.3.· Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1=miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3x31.25=miligramu 322.
Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.


Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:


1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi
2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).


3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).


4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).


5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).


6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).


7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).


8) Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.


Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.

Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.


Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokolo hii ni kazi rahisi?.


Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.


Watu wazee na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.

Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.
Kumbuka kuwa,
kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.
Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.


· Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.
·
Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).
·
Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.
·
Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.

Namna bora za kula chumvi:
· Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.
·
Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.
·
Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.
Kumbuka
chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.
Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).


Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.

Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye “multivitamins” zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.
Ili
maji yaweze kukutibu na kukukinga kwa kila ugonjwa ni lazima....
Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.


Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika:

a) Kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau, juisi ya matunda mchanganyiko, ya zabibu au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa.
Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.

b)
Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).

Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.
Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.


c) Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.


d) Hakikisha unakunywa maji kwa mjibu wa kipimo chako kulingana na uzito wako. kunywa maji mengi zaidi ya kiwango chako husababisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla hayajatumiwa na mwili.


e)
Achana kwanza kinywaji chochote cha kutengenezwa kiwandani, acha chai ya rangi na kahawa. vinywaji hivi ni mawakala vikojoshi (diuretics), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla mwili haujayatumia. utarudi kunywa chochote ikiwa utavihitaji tena vinywaji hivyo mara utakapokuwa supa tena kiafya. Acha pia uvutaji wowote wa sigara na alkoholi.

Bilashaka umewahi kusikia msemo, “Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji”, hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.

Kwanini unywe maji robo lita, robo saa kabla ya kula, au nusu lita, nusu saa kabla ya kula?:
Wanyama wote hunywa maji halisi (plain water). Ikiwa utawachunguza paka na mbwa, mara zote hunywa maji na kusubiri wastani wa nusu saa kabla ya kula. Ratiba inabadilika wanapokuwa wanatibiwa, hapa hunywa na kisha hula papo hapo ama baadaye.
Mfululizo huu ni mhimu ili kubaki na afya bora.


Unapokunywa maji na kusubiri nusu saa kabla ya kula, maji yanaenda tumboni na kuziamsha tezi kutoa kemikali (homoni) kuzifunika kuta za tumbo ili kuzirinda dhidi ya haidrokloriki asidi ambayo huzarishwa wakati chakula
kinawekwa mdomoni.

Maji na kemikali hizo kisha huenda kwenye utumbo mdogo ambako kemikali hizi hukaa kusubiri chakula kitakachokuwa kinakuja baadaye. Maji hayo huru, yanauacha utumbo mdogo na kwenda
katika seli zote za mwili na kuzijaza (kuzinyweshea) maji kama vile unavyonywesha bustani. Baada ya seli kuwa zimenyeshewa, maji yanayobaki kisha yanasukumwa tena kwenda tumboni ili kunyeshea chakula kilichofika.


Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula
, bali zinatoka katika MAJI ambayo yanaiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.

Tunatembea katika haidrojeni.


Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya.

Ikiwa haunywi maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe.
Kama
mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita 'shinikizo la damu' (BP).
Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na 'kichwa kizito' au kichwa kuuma ambacho kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.


Ikiwa unakunywa alikoholi (pombe) na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).


Watu wanaoishi katika nchi za baridi huweka alikoholi kwenye tenki zao za gesi ili kuvuta maji ndani ya gesi na hivyo kuifanya gesi isigande.


Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida kama vile kufunga choo (constipation).

kufunga choo au kupata choo kigumu sana kunatokea wakati mwili umekopa maji toka katika utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana kunakopelekea taka za mwili kusimama kwenye kuta za utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana (colon). Wakati mambo yako yanapokuwa na umajimaji, huteleza yenyewe chini bila kutumia nguvu yoyote.

Kila tunapopumuwa hewa nje (exhale) tunapoteza maji.
Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumuwa tu kila baada ya masaa 24!!.
kama mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthima) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuwaji.

Mapafu na Moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo kama mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart attack).


Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo kama unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukakamaa kwa mishipa (cramps).


Ndiyo maana wanasema; kamwe usiende kuogelea mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa itakakamaa.

Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng'enyaji chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng'enyaji wa chakula.
Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng'enywa na vinawezeshwa na maji pekee, kama vile matunda na mboga za majani.


Vinywaji vingine (liquid beverages) kama vile kahawa, chai, soda na juisi, siyo maji kwa mwili. Hivi ni vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata radha ya viongezi (additives) na siyo radha ya maji halisi, na hivyo tumbo litaitowa haidrokloriki asidi. Mwili utakishughurikia kinywaji hicho kama chakula.

Utafaidika na baadhi ya maji kama vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine). Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.
Magonjwa mengine yanayoweza kuepukika kwa kunywa maji kabla ya kula ni pamoja na vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.

Kunywa maji masaa 2 au 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng'enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng'enyaji wa chakula.

 Kunywa maji ya kawaida katika joto la kawaida.


Magonjwa mengineyanayotibika au kukingika kwa kutumia tiba ya maji ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu(BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, vidonda vya tumbo, utipwatipwa, kuzeeka mapema, na magonjwa mengine mengi.


Tiba hii ni nzuri kwa wote, wagonjwa watapona na wazima watabaki na afya bora na kujirinda dhidi ya maradhi kwa maisha yao yote.


''Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko katika dawa yeyote utakayoandikiwa na muuguzi wako – dr.Batmanghelidj''.


ANGALIZO:

· Ikiwa hauendi chooni walau mara tatu kwa siku,unapaswa kumwona daktari kabla ya kuanza tiba hii.
·
Figo zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, hii inamaanisha, kiasi cha maji unachokunywa lazima kiwe karibu sawa na unachotoa.
·
Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini mhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
·
Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia nusu ya uzito wako katika aunsi. lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha baada ya kuzoea vinywaji kama kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine.
·
Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza tiba, usiache kunywa maji kwakuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka za sumu zimeanza kuondoka mwilini, baada ya muda utarudi katika hali yako ya kawaida.
·
Tunashauri watu wenye matatizo ya figo, Ini na moyo, kutofuata tiba hii mpaka watakapopata ruhusa ya daktari na muongozo sahihi.
·
Usinywe maji zaidi ya lita 3.78 kwa siku.
·
Usinywe maji kuanzia lita moja kwa pamoja au ukiwa umekaa katika mkao mmoja iwe kusimama au kukaa.

Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.
Mr.Kikoti. Powered by Blogger.

Comments