FAHAMU HISTORIA YA DIAMOND NA ALI KIBA HAPA

By
Advertisement
 HISTORIA YA DIAMOND PLATNUMZ KWA KUZINGATIA ELIMU ALIYONAYO NA MAFANIKIO KUPITIA JUHUDI BAADA YA ELIMU


SOCIAL HALLUkitaka kujua kuwa ku-shine hapa Bongo ni juhudi zako tu mwenyewe za kupiga kazi usiku na mchana,bila kulala na mwisho wa siku kufikia malengo yako basi mfano wa kuigwa ni huyu Birthday boy Diamond Platnumz.Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam   mnamo wa saa kumi na moja na kupewa jina la  Nasibu Abdul Juma . Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote  na ikabidi wahamie Tandale Magharibi kwa bibi  yake mzaa mama, na hapo ndipo yakawa makazi yao.. Historia yake ni ya kusikitisha kama alivyoelezea kwenye wimbo wa binadamu wabaya.
Mnamo mwaka 1995  alianza kupata elimu ya Nursery katika shule ya Chakula Bora iliyopo  Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu ya Msingi yaani  (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi Tandale magharibi  iliyopo jijin Dar-es-salaam. Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano  diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kucopy  baadhi ya na kukrem nyimbo za wasanii waliokuwa wakihit ndani na nje ya  nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehem tofautitofauti.

Mara nyingi mama yake alikuwa akimnunulia kanda za album  za wasanii tofauti  waliokuwa wakihit kipindi hicho na hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za  wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, na wakati  mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofautitofauti ya tallent show  ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa  familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya  kumuhimiza kimasomo. Kiukweli hali ya maisha yao ilikuwa ni ngumu saana, maana mama Diamond hakuwa hana source ya kumuingizia kipato, hivyo  ilibidi atumie kias kidogo anachokipata toka kwa kodi ya vyumba viwili  alivyopewa na Mama yake yaani bibi yake diamond na vibiashara vyake  vidogovidogo vya mikopo kwa kumsomeshea na kumlea diamond, hakika hali  yao ya Kimaisha ilikuwa ni ngumu sana, hivyo iliwaradhimu wote kuhamia  katika chumba cha bibi huyo ili kupangisha vyumba vile viwili alivyopewa
mama diamond…


Baada ya kuhitimu shule ya Msingi mwaka 2002 na kutaka  kuanza masomo ya Secondary mwaka 2003  mama yake alimwambia aachane na
Muziki kabisa na azingatie na Masomo ili aweze kupata elimu itayomsaidia hata kwa muziki wake baadae kwa maana asingeweza kushika vitu viwili  kwa pamoja muda huo. Akiwa secondary diamond aliendelea kufanya muziki  kisirisiri bila mama yake kujua na kufikia mwaka 2004 taratibu akaanza  kujifunza kuandika nyimbo zake mwenyewe. Baada ya kuhitimu elimu yake ya Secondary mwaka 2006 mwaka 2007 alijikita rasmi katkia sughuri za  muziki ili kujaribu kutimiza ndoto zake.

kiukweli haikuwa ni safari  rahisi kama alivyotegemea hadi kupelekea time kuanza kutafuta vibarua  toafauti tofauti ili mradi aweze kupata riziki na kuepuka hali ya  kushinda nyumbani, ikiwemo kuuza mitumba, petrol station, kupiga picha,  kupigisha simu, kazi za viwandani hata wakati mwingine kuingia kwenye  makundi ya kucheza kamali za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia  studio kurecord lakini bila kufanikiwa, kiukweli ulikuwa ni wakati mgumu sana hadi ikamradhimu kuuza pete ya Dhahabu ambayo alipewa na mama yake mzazi aivae na kumdanganya kuwa ameipoteza na ndipo hapo alipofanikiwa  kuingia studio kurecord nyimbo ya kwanza iitwayo toka mwanzo..

kutokana na kutokuwa na mazoea ya kurecord hakuweza kutengeneza nyimbo ambayo ni  hit lakini wimbo ule ulianza kumpa conections tofauti tofauti maana wengi walishangazwa jinsi alivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kuweza  kutengeneza wimbo kama mtu ambae ni mzoefu, hivyo iliwafanya kuamini  kuwa akipata nafasi ya kurecord mara kadhaa angeweza kufanya kitu  kikubwa.. wimbo ule ulimfanya aweze kukutana na Chizo mapene ambae  alijitolea kumsimamia, na kweli wakaanza kurecord album lakini bahati mbaya wakiwa katikati ya kurekodi album hiyo anayemsaidia alipata  matatizo ya kifedha na hakuweza tena kumsaidia hivyo ilimbidi  Diamond aanze tena upya kuzunguka katika studio tofauti kuomba  kusigniwa kwenye record label lakini kote hakuweza kufanikiwa, wote walimwambia bado kuimba hajui na kuto kutaka kumsikiliza kabisa…
kiukweli kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana hata yule mpenzi wake ambae alikuwa nae alimuacha kwakua alikuwa ameshachoshwa na ndoto hewa ambazo  alikuwa akiziota kila siku diamond kuwa ipo siku atafanikiwa kimuziki na kuwa mwanamuziki mkubwa na wao kuish maisha mazuri, kitu ambacho kilimchanganya na kumuumiza sana diamond hususan kwa kauli aliyomuambia ya “skiza Diamond mi kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana maslahi kwangu” kutwa ilikuwa ikimpitia kwenye kichwa na kujiona kama mwenye mikosi.
Mwaka 2009,  Diamond alikutana na Bwana Msafiri Peter  maarufu  kama Papaa Misifa ambae alikubali kumsaidia kimuziki na
Kurecord wimbo wa kwanza ulioenda kwa jina la “Nenda kamwambie”, wimbo  ambao Diamond aliimba  kwa uchungu  huku akimuimbia
mpenzi wake huyo aliyemuacha (Sarah Sadiki) kuelezea kiasi  gani  aliumia kwa yeye kumuacha kwake, na hapo ndipo taratiibu nyota yake
ikaanza kung’aa na wimbo huo kukua siku hadi siku.Maisha yake yakabadilika  na Diamond kuweza  kununua gari  aina ya Toyota Celica.

Tarehe  14/02/2010 Diamond aliachia  album yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo 10 ambazo ni kamwambie  , Mbagala  , Nitarejea  , Nalia na mengi , Binadamu  , Nakupa  , Usisahau  , Uko tayari  , Wakunesanesa  , Toka mwanzo  na Jisachi. Mnamo tarehe 04 mwezi wa  4 mwaka 2010 , Diamond aliandika record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tunzo tatu za Tanzania Kili Music Awards kwa pamoja
ambazo ni: Msanii bora Chipukizi, Wimbo bora wa Mwaka (KAMWAMBIE) na  Wimbo bora wa R&B(KAMWAMBIE), tunzo ambazo zilimfanya achaguliwe  kuwa balozi wa Malaria nchini Tanzania.

Baada ya kuachia wimbo wake wa  pili  unaoitwa Mbagala,  Diamond alichaguliwa na Rais wa  jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete kuwa  Entertainer katika tour nzima ya Kampeni yake.  Tarehe 02 mwezi wa 10 mwaka 2010 alipata  tour ya kwanza kwenda England mjini LONDON,MILTON KEYNES, na COVENTRY.  Baada ya  kuachia  wimbo wake wa tatu mwaka 2011  , Diamond alishinda tuzo ya
Nzumari  Award nchini Kenya akiwa kama Msanii bora wa Kiume toka  Tanzania.  Diamond alirelease nyimbo yake ya nne na kuweka
record ya kuwa msanii wa kwanza na pekee kujaza Club Maisha hadi watu  kushindwa kuingia na hata wengine kuzimia baada kutokupata hewa ya kutosha kutokna na wingi ujaaji huo.

Mwaka mpya wa 2012, tarehe 1 mwezi wa kwanza mwaka 2012 , Diamond Platnumz aliachia album yake ya pili  na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuuza zaidi ya 1200,000 ulbum Copies. Mwanzoni mwa mwaka 2012 Diamond aliweka record ya
kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show ya Corparate iliyoitwa ” Diamons are forever” iliyofanyika Mlimani City  kwa kiinglio  cha shilingi elf hamsini 50,000  za kitanzania akiwa pekeake na show kuwa sold ot kwa zaidi ya ticket 1,500.

Mnamo mwezi wa tano mwaka 2012 , Diamond Platnumz  aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza kufanya show na kujaza zaidi ya watu 10’000 kwa kiingilio cha 20,000 katika kiwanja cha Darlive  huku akishuka na Helicopter kwenye Stage. Mwaka huohuo  Diamond alifanya
ziara yake ya Europe ikiwemo Italy, Holland, Sweden ,  Greece na kumalizia ziara yake ya arabuni nchini Masqat  Oman.

Mwishoni mwa mwaka 2012 ulikua mzuri kwa Diamond Platnumz kwani aliweza kuachia nyimbo mbili kwa mpigo za “Nataka kulewa ” na “Kesho ” zilizoambata na video zake.Mwezi wa kumi na mbili mwaka  2012 diamond alitajwa kuwa ni msanii wa kwanza anaelipwa Pesa nyingi
kwenye Show toka Tanzania


Mwanzoni mwa mwaka 2013 , Diamond  Platnumz alichaguliwa na Cocacola kuwa Brand Ambassador wa Kinywaji Cha Cocacola, na  kufuatiwa na ziara yake ya East Africa na ikiwemo Burundi  , Congo na Kenya n.k. na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza East Africa kuweza
kupiga show pekeake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000… mnamo  June 2013 Diamond alishinda tuzo mbili  za Tanzania Kili Music  Award akiwa kama   Msanii bora wa kiume Bongoflavour na Msanii bora  wa kiume kwa wanamziki wote Tanzania
Mwezi wa saba mwaka 2013 , Diamond  alirelease next single yake iliyokwenda kwa jina la Number One ambayo  aliifanyia Video Capetown South Africa Chini ya kampuni ya Ogopa  Videos  na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza kulaunch video bila  kiingilio katika Hotel ya SERENA na kuwaalika CEO’s  ,  mameneja  na  viongozi toka sehemu tofauti tofauti. katika launching hiyo akamzawadia Gari moja ya
Malegend wakubwa katika mziki wa Tanzania , Marehemu  Mwidini Gurumo.

mwezi 10 mwaka 2013  , Diamond aliifanya Collabo na msanii toka Nigeria  Davido ya ngoma ya Number one kama Remix na kisha kwenda nchini Nigeria  kwajili ya kusomea Markert ya West Africa na kushoot video ya wimbo huo  ulio shootiwa na Kampuni ya Capital Dreams iliyo chini ya Director  Clarence Peter. Nyimbo hii ilimtambulisha Diamond Platnumz nchini Nigeria na barani Africa kiujumla na kumuwezesha kupata nominations mbalimbali kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo , MTV MAMA awards ambayo aliperform nyimbo hii live na Davido, BET Awards na tuzo zinazotegemea kufanyika za AFRIMAMA , MTV Europe , Channel O awards na awards nyingine kutoka nchi mbalimbali.
Tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 2014 , wakati Diamond akisherekea Birthday ya mama yake alimzawadia mama yake gari pamoja na kuachia video mbili za mdogomdogo aliyoifanyia nchini Uingereza na BumBum aliyomshirikisha Iyanya kutoka Nigeria aliifanyia Afrika Kusini. Video hizi  kwa pamoja zilimgarimu Diamond dola 78,000 za kimarekani . Hivi Sasa nyimbo hizi ndio habari ya mjini na ni kitu kisichofikisha kwamba nyimbo hizi zitaendelea kumbeba Diamond hadi mwaka 2014 unaisha.

Huyu ndio Diamond Platnumz, mtoto wa Tandale aliyoweza kutumia kipaji chake cha kuimba vizuri, aliyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ,maisha yake ni fundisho kwa vijana kibao mjini wanaohangaika kutoka kimaisha. Familia ya Vibe Tanzania inamtakia maisha marefu wakati huu anaposherekea kutimiza miaka 26 ya maisha yake iliyousisha uchungu , mahangaiko,tabu,kutafuta na baadae kumzawadia furaha pale anapoona mafanikio yanamjia.....



HISTORIA YA ALI KIBA

SOCIAL HALL
Alikiba Saleh Kiba (born November 26, 1986) is a Tanzanian recording artiste, songwriter, dancer, producer, actor and model. He is one of Africa’s biggest stars and his name is steadily becoming a household name internationally.
So influential is Alikiba that the Tanzania’s president JakayaMrishoKikwetehonored him for his invaluable contribution to Tanzanian Music and Arts and Culture feted him.
In 2011, Alikiba was voted as “the most popular top selling artist in East Africa” – Tanzania, Kenya and Uganda by Synovate research.
His debut album, named after the hit single ‘Cinderella’ became the biggest selling record in East Africa in 2008. He followed it up with his second album “Ali K for Real” which had mega-hits like ‘Nakshi Mrembo’, ‘Nichuum’ and ‘Usiniseme’. The success of the album cemented Alikiba’s name as one of Tanzania’s all-time greats.
In 2010 Alikiba achieved another first, collaborating alongside Billboard’s “Most Influential Global R&B Artist of the past 25 years”, American singer-songwriter and record producer R Kelly for the successful One8 project alongside seven of Africa’s biggest names in music; Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio, JK.
When it comes to awards and nominations, Alikiba has them in plenty. He has been nominated for ‘Best International Act’ for Black Entertainment Film, Fashion, Television and Arts Awards, Best East African Artist (African Music Awards), Winner of Best Zouk / Rhumba Song and Best Tanzanian Writer, Best Male Artists and Best Collaborating song with Lady Jaydee (Kili Music Awards).
Alikiba Saleh Kiba was born on November 26, 1986 in Iringa, Tanzania to Tombwe Njere and Saleh Omari. He is the first of four children and is followed by Abdu Saleh Kiba, Zabibu Saleh Kiba and Abubakar Saleh Kiba.
Music has always been Alikiba’s passion since childhood. He was either going to be a soccer player or a musician but the passionfor the latter won.
During his primary school years at Upanga Primary School in Dar es salaam, he would dance and sing for his fellow students in school shows. After high school in 2004, he started pursuing a career as a songwriter and a music artist and wrote his first song, Maria. Later that year, Alikiba started working on his first album. In 2005, he received an offer from a Ugandan soccer team but turned it down to pursue and perfect his music career. As much as he loved soccer and was super talented, he loved music more and in that same year, decided to put more effort in his music.
SOCIAL HALL
2007: Cinderella Album
This was the album that introduced Alikiba to the music scene. The album’s top single, Cinderella was an instant hit and made it to number one on all of Tanzania’s music charts and was big enough to cross over to Kenya, Rwanda and Uganda.
He had East Africa’s complete attention when he followed up with even bigger hits led by MacMuga, Nakshi Mrembo and Mali Yangu. Even the Middle East could not get enough of the star. He breaking records and crossing boundaries.
2008: Alikiba 4 Real
A year later in 2008, Alikiba released his second album’s first single, Usiniseme and at this point, he was dominating the charts across East Africa and beyond. The album, Alikiba 4 Real was another piece of work from the star. In the same year, Alikiba was nominated and won the Kilimanjaro Music Awards for Cinderella.
2009: Modeling
While still soaring in his career, Alikiba received another soccer offer to play for the Tanzania soccer team, African Lyon but predictably, turned down the offer and instead decided to venture into modeling, as it didn’t take much of his time from music

0 comments:

Mr.Kikoti. Powered by Blogger.

Comments