FANYA HIVI KUONDOA MAUMIVU YA MWILI WAKO NA UDUMISHE AFYA BORA KWA MWILI WAKO
Maumivu ya nyonga huweza kuandamana naya kiuno, nyonga huunganisha miguu na mifupa ya mapaja inayotengeneza kiuno. Nyonga ndiyo inayofanya utembee kutoka sehemu moja hadi nyingine,kukimbia,kuruka,kichurachura,n.k
Maumivu ya nyonga huwa makali na husambaa hadi kwenye magoti. Ukiwa na tatizo la nyonga huwezi kufanya shughuli nyingi, mfano kuchuchumaa. Kwa wanamichezo ni adui mkubwa wa ufanisi michezoni.
Mtu anaweza kupata maumivu ya kiuno iwapo ataanguka au kupata ajali. Kiuno pia huweza kuumia kwa kuinama ghafla au kunyanyua kitu kizito. Watu wanaofanya kazi za kuinama ndiyo huathirika zaidi na tatizo hili.
Maumivu haya pia hutokea kwa kuumia vifupa vya nyonga ambapo vinaweza kuwa vimesagika au kuchoropoka. Matatizo ya nyonga pia hutokea kwa kuumia, kuteguka au kuvunjika. Uvujikaji unaweza kusababishwa na ajali yoyote, kwa kuanguka au kugongwa na gari, pikipiki au kitu kizito.
Magonjwa kama yabisi pia husababisha matatizo ya nyonga, saratani ya tezi dume kwa wanaume, saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake pia husababisha tatizo hili la kuvunjika nyonga endapo saratani hii itasambaa hadi ndani zaidi kwenye mifupa.
Kulingana na shirika la afya ulimwenguni (WHO), mtu mmoja katika ya wanane huvunjika nyonga kutokana na kuvuta sigara. Nae daktari wa mifupa anasema matumizi ya chumvi nyingi yanaweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa huo. Sababu za kuufanya mwili upoteze calcium kuwa ni kutumia kileo kupita kiasi ambacho huchangia kudhoofika kwa mifupa.
Kwa upande wa maumivu ya mgongo nyongani upande wa kushoto kuanzia juu ya makalio kwenda chini yanahusiana na mshipa wa fahamu uitwao sciatica.
Hii huwapata sana watu wanene wasiofanya mazoezi ya viungo. Isipotibiwa mapema huweza kusababisha mshituko wa moyo maana moyo unahusiana sana na mishipa ya fahamu kama vile ubongo, uti wa mgongo, ngozi na hisia pia.
MAZOEZI,
Watu wenye matatizo hayo wanapaswa kupatiwa mazoezi maalumu ili kuwasaidia kupona, kupunguza maumivu na kuwaepusha na matatizo kujirudia. Mazoezi yanayopendekezwa zaidi ni yale yanayofanywa bila kukaza sana mifupa na viungo.
Haya huanza kwa taratibu kwa mfano kutembea, kukimbia, kuogelea, kujinyoosha mara tatu au nne kwa wiki, kupanda ngazi, kucheza dansi na kuendesha baiskeli barabarani au zile maalumu zinazotumika kwenye nyumba za mazoezi (gym) Kwa upande wa kiuno na mgongo, mazoezi ni yale ya viungo maarufu kama “physiotherapy” kwa kutmia vifaa maalumu kama vile vya kujichua (massage).
Pia mazoezi mwengine ni ya kulala na tumbo kasha kuweka mikono mbele na kunyanyuka taratibu. Mgonjwa anapaswa kufanya hivyo mara kumi, pia mgonjwa aweke mikono upande akiwa amelala hivyo hivyo kasha anyanyuke taratibu afanye mazoezi haya mara kumi na mwisho aweke mikono nyuma mgongoni kasha anyanyuke tena mara kumi.
Mazoezi ya kupiga pushapu pia ni muhimu sana kwawatu wenye matatizo ya kuono na mgongo.
KUMBUKA;
- · Epuka kujitonesha kwa kufanya mazoezi haraka au kwa kutumia nguvu nyingi.
- · Epuka kubeba vitu vizito
- · Epuka kuinama ovyo au kazi ya kuchuchumaa
- · Jenga mazoezi ya kutembea mara kwa mara na epuka kukaa muda mrefu.
- · Iwapo kazi yako ni kukaa, jitahidi kila baada ya dakika 20 kunyanyuka na kutembea tembea
- · Punguza uzito
- · Kwa wanawake epuka kuvaa kiatu cha kisigino kirefu
- · Epuka kulalia godoro linalobonyea, tumia godoro maalumu la mgongo, ikiwezekana lala chini sehemu ambayo haibonyei.
- · Zingatia maelekezo ya daktari wako
0 comments:
Post a Comment