SPINAL DISC (DISC ZA UTI WA MGONGO)
ZINAVYOLETA MAJANGA
Spinal Disc ni disk zinazokaa kati kati ya pingili “Spinal Vertebrae” za uti wa mgongo. Kuna wakati disk hizo hutoka sehemu yake na kusogea pembeni tatizo ambalo linajulikana kwa majina kadhaa kama vile DEGENERATIVE DISC DISEASE au HERNIATED DISC au SLIPPED DISC. Tatizo hili husababisha maumivu makali ya mguu, mgongo, bega au Mkono. Maumivu haya huwa ni makali mno, katika mazingira mengine huuja na kutoweka, katika mazingira mengine maumivu haya huwa endelevu.
Naamini wengi wetu tumeshawahi kusikia au kuona ndugu, rafiki, jamaa, jirani fulani akiumwa mguu, mkono, bega au mgongo tena kwa maumivu makali sana.
Wengi wamehangaika hospitali nyingi bila mafanikio, wengine wamekimbilia kwenye huduma za maombezi na wengine wamekimbilia kwenye tiba mbadala na wengine wamekimbilia kwa Sangoma.
Kote huko wamekosa ufumbuzi wengine wamepoteza maisha na wengine wamepata kupooza kabisa mguu au miguu wakiwa wameshatuoa fedha nyingi sana na mateso makali.
Nilibahatika kufanya mazungumzo na baadhi ya waliowahi kupatwa na matatizo kama haya. Ndugu Selemani Mkoba alinielezea tatizo hilo lilivyomtesa na baada ya kuhangaika hospitali kwa zaidi ya miezi 3 wakati wote kiteseka kwa maumivu makali na kupoteza hela nyingi bila mafanikio aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Anasema Mganga alimpa matumaini makubwa lakini wiki kadhaa zikawa zinapita bila kupata unafuu wowote. Anasema Mgonga alikuwa akimpa matumaini kwa kumwambia ugonjwa unaingia ghafla lakini kutoka unatoka taratibu sana . Ndugu Mkoba anasema kwa bahati alipomwelezea tatizo hilo mmoja wa rafiki zake ambaye si daktari alimwambia aondoke haraka huko na kuwahi Muhimbili. Rafiki yake huyo alimweleza kuwa analifahamu tatizo hilo.
Ndugu Mkoba amasema alienda Muhimbili kama alivyoshauriwa na rafiki yake, akafanyiwa kipimo cha MRI ambapo waligundua tatizo hilo katika uti wa mgongo na kupangiwa siku ya upasuaji. Alifanyiwa upasuaji na alipozinduka alikuwa na maumivu makali ya wastani yatokanayo na upasuaji tu .. maumivu ya mguu hayakuwepo tena. Maumivu yatokanayo na upasuaji yaliendelea kupungua na sasa ni miezi mitatu amebakiwa na maumivu madogo sana mbayo yanaendelea kupoteza huku akiendelea na mazoezi. Anaweza kuendesha Gari, anaweza kutembea na kufanya shughuli zake ambazo zilisimama. Aidha Ndugu Mkoba anasema angependa watu wajue hili ili wasi mateso aliyoyapata yeye na walio kwenye mateso hayo wapate ufumbuzi haraka maana ni mateso yanayotisha.
MGAWANYIKO WA UTI WA MGONGO NA MATOKEO YA DISCK ZINAPOCHEZA
Uti wa mgongo umegawanyika katika aina kuu zipatazo nne (4) za pingili “Spinal Vertebrae”
Cervical Curve: Hili ni eneo la juu la uti wa mgongo, Eneo hili linaanzia uti wa mgongo unpokutana na kichwa na kuishia eneo la mwisho la Shingo, kwa lugha nyepesi ndilo eneo linalomiliki shingo, pingili zilizopo katika eneo hili zinaitwa “Cervical Vertebrae”.
· Maeneo yanayoathiriwa na Disc kucheza katika eneo hili “Cervical Disc Herniation” ni Mikono au Mabega au kifua, moja wapo ya viungo hivi vitapata maumivu makali sana.
Thoracic Curve: Hili ni eneo la uti wa mgongo linalofuatia kuelekea chini likianzia inapoishia Shingo, Eneo hili linaishia katikati ya mgongo, kwa lugha nyepesi eneo hili ndilo linalomilike mbavu. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Thoracic Vertebrae”.
· Kucheza kwa disck katika eneo hili kutakusababishia maumivu makali ya Mgongo eneo la juu ya Kiuno.
Lumbar Curve: Eneo hili linaanzia inapoishia Thoracic Curve na kuelekea chini na kukutana na Eneo linaloitwa Sacral Curve au eneo la kiuno linapoanzia. Eneo la Lumba linazungukwa na ma matumbo na mazagazaga mengine yasiyokuwa na mifupa. Pingili za uti wa mgongo zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Lumbar Vertebrae”
· Ikiwa Disc zitacheza katika eneo hili mhusika atapata maumivu makali ya mguu maumivu ambayo yaukumba mguuu wote kuanzia sehemu ya ndani ya tako na kushuka chini mpaka mwisho wa mguu kwenye kisigino.
Sacral Curve: Eneo hili linaanzia pale Lumbar Curve inapoishia hadi mwisho wa uti wa mgongo kwa chini. Katika lugha nepesi eneo hili ndilo linalomiliki kiuno. Pingili zinazopatikana katika eneo hili zinaitwa “Sacral Vertebrae”
SABABU ZA MATATIZO HAYA
· Ajali ya Gari
· Kuanguka
· Kupigwa/kupigana
· Michezo
· Ajali katika sehemu za kazi
· Kasoro wakati wa kuzaliwa
· Kubeba vitu vizito
· Ukaaji mbaya wa muda mrefu
· Misukosuku mbali mbali ya mwili kama
MATIBABU
Tatizo hili linatibika ikiwa mgonjwa atawahi kufanyiwa uchunguzi sahihi na tatizo hilo kugundulika. Kuna matibabu ya namna tofauuti ambayo daktari anaweza kukupa lakini hali inapokuwa mbaya Madaktari hulazimika kufanya upasuaji. Mgonjwa anatakiwa kupimwa kwa vipimo sahihi na kipimo kinachoAMINIWA zaidi ni MRI. Aidha kwa bahati Tanzania moja ya nchi chache barani Afrika zenye mitambo hii ya MRI na moja ya nchi chache barani Afrika zenye madaktari bingwa wa matatizo haya.
Wadau badala ya ya kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji tuwahi hospitali hususani Muhimbili kuonana na mabingwa wa NEURAL. Rai yangu kwa serikali pamoja na kuwa sisi tumekuwa moja katika nchi chache zenye huduma hii, mahitaji ya Madaktari hawa ni makubwa sana bado, Serikali ipeleke Madaktari zaidi nje kwa ajili ya kupatiwa ujuzi huu na kuongeza mashine za MRI angalau zifike 10.
NAMNA YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
Matunzo mazuri ya ujauzito
Kuepuka kipigana au kupigwa, usimpige mwenzako kwasababu unaweza kumsababishia tatizo baadae
Kama unaendesha gari ama piki piki kuepuka mwendo unaoweza kukusababishia ajaili
Uangalifu katika michezo na mazoezi mazito
Kujilinda kiafya ili kujiepusha na maradhi yasiyotambulika
Tujiepusha na ukaaji mbaya wa muda mrefu katika sehemu zetu za kazi, pendelea kutafuta maelekezo jinsi ya kukaa katika sehemu yako ya kazi.
Pendelea kuangalia afya mara kwa mara na kupata ushauri wa madaktari
0 comments:
Post a Comment