Uchumi ni jumla ya shughuli zote za kibinadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji ya watu. Ni hasa shughuli za uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.
Uchumi mara nyingi hutazamiwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia.
Uchumi Mkuu: (macroeconomics) ni elimu juu ya picha kamili ya uchumi, yaani njia ambayo utajiri unapatikana na unagawanywa. Inaweza kuwa elimu kuhusu nchi maalum au dunia nzima na jinsi tofauti zinavyoingizwa katika picha nzima ya dunia. Kuna majadiliano kama ya:
|
Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kuwa masikini zaidi. Tufanye nini kuhusu jambo hili?
|
|
Serikali ijiingize kiasi gani katika uendeshaji wa soko huru?
|
|
Kwa kuzingatia na uharibifu wa mazingira, je, ukuaji wa uchumi usiodhibitiwa unatakiwa?
|
Uchumi Mkuu Imara (Macroeconomic Stability) ni matokeo ya kuwa na kodi ya hazina, sera za fedha na kiwango cha kubadilishana fedha inayokusudia kufikia malengo ya uchumi mkuu kama vile ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, madeni ya nje na akiba halisi ya kimataifa.
Uchumi Mdogo (Microeconomics) ni elimu kuhusu jinsi viwanda, sekta fulani, biashara au kaya zinavyofanya kazi.
Jumla ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product - GDP) ni kipimo cha jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana nchini katika muda maalum. Kwa maneno mengine Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa fedha. Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1% zaidi kuliko ya mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1%. Lakini jumla ya pato la taifa (GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa – kwa mfano, uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi yao.
Jumla ya Pato la Taifa (GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.
Ukuaji Halisi (Real Growth): Kwa vipengele vyote viwili jumla ya pato la utajiri (GDP) na ukuaji wa pato la utajiri (GNP), kama ukuaji ni asilimia 7% kwa mwaka, lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5% basi Ukuaji Halisi ungekuwa asilimia 2% tu kwa mwaka.
Mfumuko wa Bei (Inflation): Kipimo cha kupanda kwa bei kati ya mwaka mmoja na mwaka unaofuata – hasa ukizingatia wazo la kupata vifaa vya madukani/sokoni.
Mtaji wa jamii (Social Capital) ni kama “gundi” inayounganisha pamoja familia, makundi na jumuiya. Inahusisha imani, desturi na tabia za jamii ambazo husaidia kufanya kazi pamoja kwa uthabiti katika makundi yaliyo rasmi na yasiyo rasmi.
Vyama vya Jumuiya (Civil Society Organisation):Inahusisha vyama rasmi ambavyo vimesajiliwa na serikali na vile visivyo rasmi. Vyama hivyo ni pamoja na vile vya hisani, dini, vya shughuli maalumu, kundi shawishi, kitaaluma, na vyama vya makundi maalumu kama vile vyama vya wafanyakazi na vyama vya wanafunzi. Vyama visivyo rasmi ni pamoja na Upatu, vyama vya makabila, mpira wa miguu ambavyo vinaundwa na vijana wa kiume na netiboli vinavyoundwa na vijana wa kike.
Matayarisho Ya Bajeti inayozingatia maskini (Pro-poor Budgeting): na usimamizi wa matumizi (and expenditure monitoring). Fedha zinatengwa katika bajeti kwa ajili ya programu zinazowalenga watu masikini. Lakini fedha hizi zinapaswa kupitia Hazina, wizara inayohusika, serikali za Mikoa na Halmashauri za Wilaya/ Miji na kitengo cha huduma (k.m. shule au hospitali) kabla ya mtu masikini kupata faida. Kwa usimamizi thabiti fedha hizi zinaweza kutumika vizuri.
Mapitio ya Matumizi ya Serikali (Public Expenditure Review). Timu ya Matumizi ya Serikali hukutana mara moja kila baada ya majuma mawili ili kutafakari jinsi serikali inavyopata na kutumia fedha zilizo kwenye bajeti. Timu hii iliundwa mwaka 1997 inawajumuisha viongozi wakuu wa serikali na wawakilishi kutoka katika jumuiya ya wafanyabiashara, makundi ya jumuiya na makundi ya wafadhili wa nje.
Bajeti za Serikali (Government Budgets). Serikali ni kama familia ambayo inapaswa kuweka uwiano kati ya fedha zinazoingia na fedha zitumikazo. Kama hakuna fedha zinazoingia serikali inapaswa kuamua itumie kiasi gani na isitumie kiasi gani. Utaratibu wa kukusanya taarifa hii na kufanya uamuzi ndiyo huitwa Bajeti
Njia za Mapato ya Serikali (Source of government income):
| Kodi ya moja kwa moja k.m. kodi ya mapato, kodi ya mali |
| Kodi isiyo ya moja kwa moja k.m. kodi ya ushuru wa forodha, kodi ya mauzo |
| Mapato yasiyo na kodi k.m. liseni na ada |
| Mikopo k.m. toka Mashirika ya Fedha Duniani na Benki ya Dunia · |
| Misaada k.m. toka serikali nyinginezo na toka mashirika yasiyo ya kiserikali |
Kuongeza kodi ni jambo lisilopendwa na baadhi ya kodi nyingine ni mzigo mkubwa kwa watu masikini kuliko watu matajiri. Mikopo ni mizuri kuziba mapengo ya muda mfupi na kuanzisha biashara mpya, lakini lazima mikopo hiyo ilipwe. Misaada inakaribishwa bali hatuwezi kupata misaada wakati wote.
Mishahara na Gharama Nyinginezo (Personal Emoluments (PE) and other charges (OC)): Wizara inatumia sehemu ya bajeti yake kwa mishahara na sehemu nyingine kulipia gharama nyinginezo. Kama sehemu ya kutekeleza waraka wa Upunguzaji wa Umasikini (PRSP), Serikali itaongeza bajeti ambayo inatengwa kwa ajili ya gharama za matumizi mengine – kwa mfano, kati ya mwaka 1999/2000 hadi 2002/2003 bajeti itaongezwa toka asilimia 2 hadi 3.8% kwa ajili ya elimu ya msingi na toka asilimia 2.1 hadi 3.8% kwa ajili ya Afya ya Jamii.
VIFUPISHO VYA KIUCHUMI
BoT Bank of Tanzania – Benki Kuu (ya Tanzania)
CAS Country Assistance Strategy – Mbinu za Kusaidia Nchi
CSO Civil Society Organisation – Jumuiya Hiari za Wananchi
DED District Executive Director – Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
ELCT Evangelical Lutheran Church of Tanzania – Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
ESAF Enhanced Structural Adjustment Facility – Uharakishaji Mabadiliko ya Kimuundo
GDP Gross Domestic Product – Pato Ghafi la Ndani
GNP Gross Nationa Product – Jumla ya Pato la Taifa
HBS Household Budget Survey (1991/92) – Mapitio ya Bajeti za Kaya (1991/92)
HIPC Highly Indebted Poor Countries – Nchi Masikini zenye Madeni Makubwa
HRDS Human Resource Development Survey (1993) – Ukaguzi wa Maendeleo ya Nguvu kazi (1993)
HRS Human Resource Survey (1983) – Ukaguzi wa Nguvu kazi
IBRD International Bank for Reconstruction and Development (World Bank) – Benki ya Dunia ya Urekebishaji na Maendeleo
IFMS Integrated Financial Management Information System – Mfumo wa Pamoja wa Taarifa za Uendeshaji wa Fedha
IMCI Integrated Management of Childhood Illness – Uendeshaji wa Pamoja wa Magonjwa ya Watoto
IMF International Monetary Fund – Shirika la Mfuko wa Fedha Duniani
LGRP Local Government Reform Programme – Mpango wa Mageuzi wa Serikali za Mitaa
M & E Monitoring and Evaluation – Usimamizi na Tathmini
MDF Multilateral Development Fund – Mfuko wa Shughuli mbali mbali za Maendeleo
MSME Micro, Small and Medium Enterprises – Viwanda Vidogo na vya Kati
MTEF Medium-term Expenditure Framework - Muundo wa Matumizi ya Muda wa Kati
NBS National Bureau Statistics – Kitengo cha Taifa cha Takwimu
NGO Non-Government Organisation – Shirika lisilo la Kiserikali
NPES National Poverty Eradication Strategy – Mpango wa Taifa wa Mkakati waKupunguza Umasikini
OPM Oxford Policy Management – Manejimenti ya Oxford kuhusuSera ya Uongozi
PER Public Expenditure Review – Mapitio ya Matumizi ya Serikali
PL Poverty Line – Mstari wa Umasikini
PMI Poverty and Welfare Monitoring Indicators – Viashirio vya Uratibishaji wa Umasikini na Usawa
PPA Participatory Povery Assessment (1995) – Tathmini ya Ushirikishwaji juu ya Umasikini
PRGF Poverty Reduction and Growth Facility – Mfumo wa Ukuaji na Upunguaji wa Umasikini
PRSC Poverty Reduction Support Credit – Mikopo ya Kusaidia Kupunguza Umasikini
PRSP Poverty Reduction Strategy Paper – Mkakati wa Mbinu za Upunguzaji Umasikini
PSAC-I Programme Structural Adjustment Credit – Programu ya Mikopo ya Urekebishaji Miundo
PSRP Public Service Reform Programme – Programu za Mageuzi ya Huduma za Umma
RAS Reginal Administrative Secretaries – Makatibu Tawala wa Mikoa
SME Small to Medium Enterprises – Viwanda Vidogo hadi vya Kati
TAS Tanzania Assistance Strategy – Mbinu za Kusaidia Tanzania
TIC Tanzania Investment Centre – Kituo cha Uwekezaji Tanzania
TIPER Tanzania-Italian Petroleum Refinery – Mtambo wa Kusafisha Mafuta Tanzania na Italia
TRCHS Tanzania Reproductive and Child Health Survey (1999) - Mpango wa Uzazi na Afya ya Watoto
TSED Tanzania Socio-Economic Database – Mfumo wa Utunzaji wa Taarifa za Jamii na Uchumi
TTC Teacher Training College – Chuo cha Ualimu
VPO Vice President's Office – Ofisi ya Makamu wa Rais
|
0 comments:
Post a Comment