Moja kati ya matatizo ya zama hizi kwa watumiaji wa simu ni uwezo wa simu zao kukaa na chaji. simu zinakaa na chaji kwa muda mchache kiasi kwamba inabidi wajinyime matumizi waache kufanya vitu fulani ili simu iweze kukaa angalau siku moja. ili kupambana na hili tatizo nimeandaa hii makala ili mpaka mtu akimaliza kuisoma awe na uelewa juu ya battery na chaja na wakati mwengine aweze kuchagua simu anayoitaka mwenyewe.
BATTERY YA SIMU
kwa wasiofahamu battery ya simu hiki ndio kifaa kinachotunza nguvu ya umeme inayotumiwa na simu yako na mara nyingi inakaa nyuma ya simu na zipo battery za simu zinazotoka na zisizotoka.
UJAZO WA BATTERY
hapa ndio pa muhimu sana, battery yako ikiwa na ujazo mkubwa basi kuna uwezekano mkubwa wa simu yako kukaa na chaji sana. ujazo wa battery ya simu unapimwa kwa milli ampere hour au kwa kifupi mah. ina maana simu ikiwa na mah kubwa basi itakaa sana na charge kuliko yenye mah ndogo.
hebu tuangalie mfano hai una gari, gari yako ina tank la mafuta na ujazo wa mafuta kwenye gari unapimwa kwa lita. hivyo unaweza kusema gari langu lina tank kubwa la mafuta hivyo linaweza kwenda safari ndefu bila kujaza mafuta ikiwa full tank.
1. gari = simu
2. tank la mafuta = battery ya simu
3. lita za mafuta = mah
hivyo kwa mfano huo hapo juu tunaona simu inahitaji battery yenye mah nyingi ili kukaa sana na charge.
UIMARA WA BATTERY
uimara wa battery unatokana na cell zilizotumika kutengenezea hio battery. cell imara zinaruhusu kuchajiwa mara nyingi bila kuharibika. kuna battery unaweza kuzichaji hata mara 1000 zisipoteze ubora wake zikawa bado nzima ila battery nyengine ukizichaji mara 50 au 100 tayari zinaharibika. ni vigumu kujua kama battery hii ina cell imara au ambazo sio imara hivyo ni vyema ukitaka battery imara uinunue kwa makampuni yanayojulikana. wale wanaonunua power bank hii pia inawahusu.
OPTIMIZATION YA BATTERY
turudie mfano wetu wa gari tumesema ukiwa na lita nyingi za mafuta basi na gari litaenda umbali mrefu lakini je hili ni kweli 100%?? kuna magari yanakunywa mafuta sana na mengine hayanywi mafuta sana na hili inategemea jinsi kiwanda kilivyo optimize mashine.
kwenye simu mambo yapo hivi hivi kuna simu zina mah kubwa lakini zinakaa na chaji kidogo na simu zina mah ndogo zinakaa na chaji sana na hili linatokana na jinsi watengeneza simu walivyoeka hardware na software zao vizuri. hapa tuchukulie simu nne kama mifano mbili za windows phone na mbili za android, lumia 1520, lumia 1320, galaxy note 3 na xperia t2.
lumia 1520 na lumia 1320 zote mbili zina battery yenye ukubwa wa 3400mah. lumia 1520 ina kioo full hd na processor yenye kasi kuliko lumia 1320 lakini linapokuja suala la kukaa na chaji lumia 1520 inakaa sana na chaji hivyo hapa inaonesha simu zinaweza kuwa na battery sawa ila zikatofautiana muda wa kukaa na chaji
hivyo hapo utaona kuna utofauti mkubwa karibia masaa 32 japo battery zipo sawa.
tukija kwenye android kuna galaxy note 3 na sony xperia t2. galaxy note 3 ina 3200mah wakati xperia t2 ina 3000mah kwa macho ya kawaida utaona note 3 ni bora hebu tuangalie benchmark zinasemaje.
hivyo unaona japo xperia t2 ina battery ndogo ila imeipita note 3.
kwa ushauri zaidi inabidi mtu uangalie simu yenye mah nyingi halafu pia uangalie na review yake ya battery.
EXTENDED BATTERY
tumeiangalia battery vizuri na hadi hapa utakua na idea ya kutosha kuhusu battery kwa nyongeza ni kwamba unaweza kubadili simu yako yenye battery ndogo ikawa kubwa. mfano simu yako inakuja na battery ya 1500mah unaweza ukanunua battery nyengine ya 3000mah ili kuongeza muda wa simu kukaa na chaji.
CHAJA ZA SIMU
umeshawahi kutumia chaja moja ikawa inachaji simu upesi na nyengine ikawa inachaji kidogo dogo? hili tatizo linatokana na kuchajia chaja ambayo ina ampere ndogo. ampere ndio inayokujulisha kiasi gani cha umeme kinaingia kwenye battery na kifupi chake ni herufi A. nitajaribu kuzieka chaja na aina za simu
- 0.15A-feature phone
- 0.45A-usb2.0 charging
- 0.5A-smartphone ndogo
- 0.9A-usb3.0 charging
- 1A-smartphone kubwa
- 2A-tablets
hivyo inabidi kabla hujanunua chaja kwanza angalia battery yako inataka ampere ngapi halafu ununue na chaja ambayo ina ampere kama battery yako. pia unapotumia charger yenye ampere kubwa na voltage zile zile kama battery yako basi simu itajaa chaji mapema zaidi..
source;CHIEF MKWAWA
0 comments:
Post a Comment