10 BORA YA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI,SHULE ZILIZOFANYA VIZURI ,NA SHULE ZILIZOSHIKA MKIA KATIKA MATOKEO CSEE2015

By
Advertisement

Baraza la Mitihani (NECTA) leo Februari 18, 2016 limetoa Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.

Jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.

Upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).

Upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12 waliofaulu mwaka 2014.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, amesema waliopata daraja la Kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.

Waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wavulana 38,338 sawa na asilimia 19.63

10 BORA YA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015.



1.Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani
2.Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam
3.Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani
4.Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya
5.Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro
6.Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani
7.Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
8.Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa
9.Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
10.Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys


HIZI NDIO SHULE KUMI BORA ZILIZOONGOZA KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015


1.Kaizirege mkoa wa Kagera
2.Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
3.Marian Boys mkoa wa Pwani
4.St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
5.Abbey mkoa wa Mtwara
6.Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
7.Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
8.Marian Girls mkoa wa Pwani
9.Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

SHULE 10  ZILIZOSHIKA MKIA KATIKA MATOKEO  YA KIDATO CHA NNE 2015


Manolo mkoa wa Tanga
Chokocho mkoa wa Pemba
Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam
Mashindei mkoa wa Tanga
Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
Vudee mkoa wa Kilimanjaro
Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro
Magoma mkoa wa Tanga.


0 comments:

Mr.Kikoti. Powered by Blogger.

Comments